Rwanda : Mahakama yamuondolea Dieudonné Ishimwe mashtaka ya ubakaji
Mahakama ya Kigali imefuta kesi ya ubakaji dhidi ya mwandalizi wa mashindano ya Miss Rwanda, Dieudonné Ishimwe, ila mahakama hiyo imesema Ishimwe atashtakiwa kwa makossa mengine yanayohusiana na unyanyasaji wa kingono.
Imechapishwa:
Mahakama hiyo pia imemunyima Ishimwe dhamana baada ya kumatwa kwake mwezi uliopita, akihusishwa na madai ya kuwanyanyasa kingono wasichana wanaoshiriki mashindano ya Miss Rwanda, mashtaka ambayo ameyakanusha.
Mahakama imesema hakuna ushahidi wa kutosha kumfungulia Ishamwe mashtaka ya ubakaji, ila anaweza kufunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono.
Shuktama dhidi ya Ishimwe ni miongoni mwa mijadala ambayo inagonga vichwa vya habari nchini Rwanda, baadhi ya raia wakihusisha mashataka hayo na siasa, serikali nayo ikilazimika kufuta mashindano ya mwaka huu ya Miss Rwanda kutokana na shutama hizo.