Pata taarifa kuu
KENYA-UINGEREZA-UKOLONI

Koo ya Talai nchini Kenya yataka Uingereza kuiomba radhi kwa kuwatesa

Nchini Kenya, watu zaidi ya 100,000 kutoka koo ya Talai katika Kaunti ya Kericho, wamemwandikia barua mwanamfalme William wa Uingereza, kutaka waombwe radhi, kufuatia mateso waliyopitia wakati wa kipindi cha ukoloni kabla ya kupata uhuru mwaka 1963.

Kipindi cha ukoloni nchini Kenya
Kipindi cha ukoloni nchini Kenya ThisIsAfrica.me
Matangazo ya kibiashara

Kupitia wakili wao, Joël Kimutai Bosek, watu hao wanasema wamepitia kwa MwanaMfalme William baada ya madai hayo kuupuzwa na serikali ya Uingereza.

Watu hao wanadai walifukuzwa katika mashamba yao katika Kaunti ya Kericho kati ya mwaka 1902 hadi 1963, lakini pia haki zao kudhulumiwa, ikiwa ni paloja na wanawake kubakwa na wanaume kuzuia na hata kuuawa.

Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa kwa MwanaMfalme William, watu hao wanataka Uingereza itambue yote yaliyofanyika na kuwaomba radhi na wanapitia kwake kwa sababu ya uhusiano binafsi alionao na nchi ya Kenya.

Serikali ya Uingereza inasema tayari imeshawaomba radhi wakenya mwaka 2013 kwa mateso yaliyotokea wakati wa kipindi cha ukoloni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.