Pata taarifa kuu
KENYA-MAOMBOLEZO

Kenya: Mazishi ya kitaifa kumwaga rais wa zamani Mwai Kibaki yafanyika

Nchini Kenya, maefu ya raia wa nchi hiyo wameugana na viongozi mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika kwenye mazishi ya kitaifa  kumwaga aliyekuwa rais wa tatu Mwai Kibaki, aliyefariki dunia wiki moja iliyopita akiwa na miaka 90.

Wanajeshi wa Kenya wakiwa wanavuta mwili wa aliyekuwa rais wa tatu wa nchi hiyo, Hayati Mwai  Kibaki wakati wa mazishi ya kitaifa jijini Nairobi. 29/04/2022
Wanajeshi wa Kenya wakiwa wanavuta mwili wa aliyekuwa rais wa tatu wa nchi hiyo, Hayati Mwai Kibaki wakati wa mazishi ya kitaifa jijini Nairobi. 29/04/2022 © StateHouseKenya
Matangazo ya kibiashara

Mazishi hayo yamefanyika jijini Nairobi, kuelekea kuzikwa siku ya Jumamosi.

Mwandishi wetu Hillary Ingati alihudhuria mazishi hayo na kuandaa ripoti hii :

Mamia ya raia waliaanza kuwasili katika uwanja huu mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi Afrika Mashariki wakitokea pembe tofauti za nchi.

Mazishi ya kitaifa kumwaga aliyekuwa rais wa tatu wa Kenya Mwai Kibaki (29/04/2022)
Mazishi ya kitaifa kumwaga aliyekuwa rais wa tatu wa Kenya Mwai Kibaki (29/04/2022) © StateHouseKenya

Baadhi ya wanachi waliofika hapa, watoto kwa wazee, wamekumbuka Hayati Kibaki kwa njia tofauti.

 “Masomo yangu ya kwanza yenye kibaki aliaanza ya bure nilikuwa mojawao mwaka wa kwanza.”

 “Alifanya mama aende shule.”

“2002 akiingia ndio nilikuwa naenda shule ya chekechea kwa hiyo miaka yote hadi mwaka wa 2013 nimesoma bila kulipa karo, mama hakuwa na kitu sasa bila yeye singepata elimu”

 “Mzee ameawacha historia mabarabara hiyo yote, daraja na hii barabara ya gorofa kenya haikuwa imeona tumeona vitu vingi kibaki alifanya”

 “Huyu Mzee alitupea elimu ya msingi ya bure, wacha hii wanasema ni bure siku hizi hakuna bure lazima ulipe, ati wakati wa kibaki upange laini ununue mafuta ?  Kibaki angesema huo ni upumbavu watu wapewe mafuta kenya iko na mafuta”

Aliyekuwa waziri mkuu katika serikali ya kibaki, Raila Odinga naye pamoja na naibu rais wa sasa William Ruto nao pia wamemuenzi hayati kibaki …

 “Kila wakati amekuwa mshauri wangu na nimepoteza rafiki, taifa la kenya limepoteza mtu mzalendo, kiongozi bora zaidi ambaye umuhimu wake utasalia kumbukwa kadir muda unavyosonga pumzika salama rais kibaki” alisema Odinga.

 “Rais Kibaki na historia yake, ni historia ya taifa letu , Alikuwa mojawapo watu waliopanga upatikanji wa uhuru wetu , alikuwa moja wa watu waliounda serikali yetu ya kwanza na alitoa mchango mkbuwa sana na akawa mwazilishi wa uchumi wetu” alisema Ruto.

Ujumbe wa rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, Umesomwa na waziri wake wa mambo ya kigeni. “Wakati rais Kibaki alishika hatamu kutoka kwa rais Daniel Moi, alihakikisha kuwa mchakato wa kuleta amani  uliopelekea kutiwa saini kwa makubaliano ya amani ya amani mwaka wa 2005 yalizingatia matakwa ya watu wa sudan kusini”

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta naye ametaja mtangulizi yake kama mtu wa kupenda amani.

 “Tunamsherekea mtu wa imani, Mtu wa Heshima na mtu aliyeeka kenya na wakenya kwanza kwa hivyo hata kama rais kibaki amepumzika, Matendo yake mema kwa nchi yetu  hayatapumzika hadi wakatu ule maono yake kwa taifa hili yatatimia” alisema Kenyatta.

Ibaada hiyo pia imehudhuriwa na marais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Saleh Wakzued wa Ethiopia, Naibu rais wa Tanzania Philip Mpango, Waziri Mkuu wa Rwanda Edward

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.