Pata taarifa kuu
TANZANIA-AJALI

Ajali ya barabarani yaua zaidi ya 20 nchini Tanzania

Watu 23 wamefariki dunia na wengine 38 kujeruhiwa nchini Tanzania, baada ya ajali ya barabarani kuhusisha basi la abiria na lori, katika mkoa wa Morogoro siku ya Ijumaa.

Ramani ya Tanzania ikionesha Morogoro
Ramani ya Tanzania ikionesha Morogoro AFP
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo imetokea eneo la Malela, Kibaoni wilayani Mvomero huko mkoani Morogoro baada ya lori lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda DR Congo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Ahmeed.

Kamanda wa polisi katika mkoani Morogoro Fortunatus Muslim, amesema lori hilo liliacha njia wakati likijaribu kumpita mwendesha pikipiki, wakati lilipogongana na Basi hilo la abiria lililokuwa linakwenda mjini Dar es salaam , likitokea Mbeya.

Aidha, kamanda Kamanda Muslim ametahadharisha kuwa idadi ya vifo inaweza, kuongezeka.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza jamaa zao katika ajali hiyo na kutoa wito kwa watumiaji wa barabarani kuheshimu sheria za barabarani.

Ajali kama hizi zimekuwa zikitokea nchini Tanzania, sababu kubwa ikielezwa ni kwa madereva kutoheshimu sheria za barabarani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.