Pata taarifa kuu
KENYA-SIASA

Siku ya Kimataifa ya wanawake duniani: Siasa na wanawake nchini Kenya

Kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9 nchini Kenya, mashirika ya kutetea haki za binadaam yanahofia dhulma za kijinsia huenda zikaongezeka, hali inayozidi kuwapa wasi wasi wanawake wanaotarajia kuwania nafasi mbalimbali.

Bunge la Kenya jijini Nairobi
Bunge la Kenya jijini Nairobi REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Katika majengo ya bunge ya Kenya ,wabunge hao akina mama wameondoka kwenye vikao vya alasiri ,kukashifu kitendo cha mwenzao kuzabwa Kofi na mbunge mwenza wa kiume.

Ibara ya nne ya Katika inahusu haki na imewapa jinsia zote haki ya kuchaguliwa kwenye nafasi yoyote, hata hivyo wanawake huisi haki hiyo hawajahikishiwa kutokana na dhulma za kijinsia.

Farhiya Ali ni seneta kutoka Wajir na naibu kinara katika Bunge la Senate, yeye ashawahi kupigwa .

 “Nilikuwa baraza  Wajir,nikaongea kuhusu ufisadi,msichana akakuja akanipiga kofi,mimi nikaona tu ametumwa,”alisimulia Seneta Farhiya Ali.

Millie Odhiambo, mbunge  katika bunge la kitaifa tangu mwaka 2008, anasema ashawahi kuchomewa nyumba wakati wa uchaguzi, picha zake kutumika vibaya, akitaka wanawake kulindwa zaidi.

Waweke police unit ya kipekee ya wamama wako kwa siasa,Kama êneo bunge langu  iwe  polisi kama watano,”alishauri Millie Odhiambo.

Wanawake wanaoingia katika siasa kwa mara ya kwanza, tayari wanajiskia kukata tamaa Patience Nyange amejitosa kwenye kinyanganyiro cha ugavana, kaunti ya Taita Taveta, Pwani ya Kenya.

Nana anakufadhili kwenye hii siasa? Wewe umeolewa wapi? Wewe bwanako ni nani? Una watoto wangapi? Wananza kukuwekea vigezo vingi, ili useme  aah kama hujaolewa kwenye hii jamii wewe si wetu,kama wewe bwana wako si  wa jamii yetu ,wewe si wetu ,basi kama wewe huna watoto unawalea basi hujatosha kwa uongozi,” alisikitika Patience Nyange.

Mashirika ya kutetea haki za wanawake kwa upande wao, wanaendelea kuwaanda wagombeaji wanawake, Nancy Ikinu ni mkurugunzi wa shirikisho la mawakili wanawake nchini Kenya.

“ Tumeleta watalaam  wale wataonge na akina mama kujitayarisha kuchukua uongozi,” alisema Nancy Ikinu.

Dhulma za kijinsia ni hatia  katika sheria za  Kenya  na zinajumuisha  dhulma za kupigwa ,ubakaji na hata kutukanwa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.