Pata taarifa kuu
TANZANIA

Magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa nchini Tanzania, yarejeshwa

Nchini Tanzania, serikali imetoa leseni mpya kwa magazeti manne ya Mwanahalisi, Mawio, Tanzania Daima na Mseto ambayo yalikuwa yamefungiwa.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan - AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Leseni hizo mpya zimetolewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ambaye amesema hatua hii imekuja kwa sababu serikali nchini humo ina kutengeneza na kujenga mahusiano mazuri na waandishi wa habari.

Magazeti hayo yalifungiwa kwa nyakati tofauti wakati wa uongozi wa Marehemu John Magufuli, ambaye alishtumiwa kuminya uhuru wa vyombo vya Habari nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.