Pata taarifa kuu

Vifo vya wafungwa Gitega: HRW yainyooshea kidole cha lawama Gitega

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema serikali ya Burundi bado haijafanya uchunguzi huru na wa kuaminika baada ya wafungwa kuuawa na wengine kujeruhiwa wakati Gereza la mji mkuu wa Gitega lilipoteketea kwa moto mwaka uliopita. 

Gereza la Gitega, mji mkuu wa Burundi, lililoteketea kwa moto mkubwa Desemba 7, 2021.
Gereza la Gitega, mji mkuu wa Burundi, lililoteketea kwa moto mkubwa Desemba 7, 2021. © AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch inashtumu serikali ya Burundi kwa kushindwa kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo lilotokea Desemba 7 na kusababisha vifi vya wafungwa 38 na wengine 69 kujeruhiwa kwa mujibu wa taarufa zilizotolewa na serikali. 

Mkurugenzi wa Shirika hilo katika eneo la Afrika ya Kati Lewis Mudge, amesema kukosekana kwa taarifa za uhakika na kushindwa kutoa idadi kamili ya watu walioangamia kwa kuwataja majina pamoja na wale waliojeruhiwa, inaendelea kuzua maswali mengi. 

Human Rights Watch, inasema ni lazima serikali ya Burundi ieleze chanzo cha moto huo katika gereza hilo lililokuwa na wafungwa kupita kiasi, iwachukulie hatua waliohusika na iwalipe fidia família za wafungwa walioangamia. 

Shirika hilo linasema, liliwahoji walionusirika katika mkasa huo na waliotembelea gereza hilo na huenda mamia ya wafungwa waliuawa na wengine kujeruhiwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.