Pata taarifa kuu

Umoja wa Ulaya wajiandaa kuondoa vikwazo vyake vya kiuchumi dhidi ya Burundi

Umoja wa Ulaya, uliokuwa umetangaza kuongeza muda wa kuendelea kuiwekea vikwazo vya kiuchumi nchi ya Burundi, imeamua kuondoa vikwazo hivyo dhidi ya taifa hilo linaendelea kupitia kipindi kigumu cha kiuchumi.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye mwezi Juni 2020.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye mwezi Juni 2020. AFP - TCHANDROU NITANGA
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema, serikali ya Burundi sasa inasubiri taarifa rasmi kutoka kwa umoja wa Ulaya, huku afisa mmoja ambaye hakutaka jina lake kutajwa, akisema ni habari njema sana kwa serikali ya Gitega.

Umoja wa Ulaya ulikuwa umeiwekea Burundi vikwazo hivyo kwa miaka metano kwa sababu ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu na masuala ya kisiasa, na hivi karibuni iliongezewa muda baada ya kutokuwepo kwa mwafaka wa pamoja ndani ya Umoja huo lakini, kwa sasa suluhu imepatikana

Duru nyingine imesema hatua hii imekuja baada ya rais Evariste Ndayishimiye, kuonesha nia ya kuimarisha demokrasia na haki za binadamu baada ya mzozo wa mwaka 2015, hatua ambayo pia imesababisha kuanza tena kwa mazungumzo ya kisiasa tangu mwezi Februari.

Hata hivyo mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, Maria Arena, anasema hatua ya serikali ya Burundi kumkataa mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, ingekuwa ishara ya kutoondelewa kwa vikwazo hivyo lakini akaongeza, uamuzi upo mikononi kwa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.