Pata taarifa kuu

Burundi: Makumi wauawa katika mkasa wa moto katika jela kuu la Gitega

Nchini Burundi, gereza kuu la mji mkuu Gitega limeharibiwa na moto mapema Jumanne asubuhi. Takriban watu 38 wamefariki dunia na 69 wamejeruhiwa vibaya, kwa mujibu wa makamu wa rais wa Burundi aliyetembelea eneo la tukio, akiwa mkuu wa ujumbe wa serikali.

Mji mkuu wa Burundi, Gitega.
Mji mkuu wa Burundi, Gitega. Wikimedia Commons / Public Domain
Matangazo ya kibiashara

Prosper Bazombanza, na mawaziri wake wanne (ule wa Mambo ya Ndani, Haki, Afya na Mshikamano) walikuwepo katika eneo la tukio leo asubuhi kuangalia uharibifu uliosababishwa na moto huo katika jela kuu la Gitega.

Chanzo cha moto huo bado hakijabainika. Inasemekana kuwa moto huo ulizuka mwendo wa saa 10 asubuhi kwa saa za Burundi, na kuwashtukiza wafungwa wakiwa usingizini. Mashahidi wamethibitisha kwa shirika la habari la AFP kwamba waliona moto mkubwa ukitokea na kuteketeza kabisa sehemu za jengo la gereza.

Jela lenye msongamano wa wafungwa

Mmoja wa wafungwa ambaye ameweza kuongea kwenye simu amesema alipiga kelele "tutachomwa moto tukiwa hai, lakini, ameongeza, polisi walikataa kufungua milango ya sehemu tulikuepo, wakisema" haya ni maagizo ambayo tumepokea ". Wafungwa wenzake waliteketea kwa moto akisuhudia kwa macho yake.

Kwa mujibu wa mashuhuda wengine, wazima moto walifika saa mbili baada ya kuzuka kwa moto huo, kabla ya majeruhi karibu 20 kuondolewa na kupelekwa hospitalini. Mwezi Agosti, mkasa mwingine wa moto ulizuka katika gereza la Gitega kutokana na kasoro za umeme, lakini moto huo haukusababisha hasara yoyote. Kwa sasa idadi ya vifo ni kubwa na jela hilo lina wafungwa 1539 kwa vitanda 400 pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.