Pata taarifa kuu
RWANDA

Rwanda: serikali yalegeza hatua za kudhibiti Covid-19

Hali ya kawaida yarejea nchini Rwanda, baada ya mwaka mmoja na nusu nchi hiyo ikiwa chini ya hatua kali dhidi ya Covid-19. Rwanda tamewapa chanjo zaidi ya watu milioni 1.5, wakati idadi kama hiyo mara mbili zaidi tayari wamepokea dozi ya kwanza. Na kesi za maambukizi na vifo zimepungua.

Wahudumu wa afya kiyuo cha Center Biomedical cha Kigali wakipima Covid-19, Julai 28, 2020.
Wahudumu wa afya kiyuo cha Center Biomedical cha Kigali wakipima Covid-19, Julai 28, 2020. AP
Matangazo ya kibiashara

Wiki hii, serikali iliondoa marufuku ya wasafiri wanaoingia nchini Rwanda. Na kisha baadaye ikatangaza kufunguliwa hatua ka hatua kwa kumbi za michezo, mabwawa ya kuogelea na kusogeza sheria ya kutotoka nje hadi usiku wa manane. Baa zilizoanza tena shughuli zao wiki chache zilizopita sasa zinaweza kuwakaribisha wateja baadaye kidogo.

Mlolongo wa magari

Mbele ya mgahawa wa Coco Bean, kumeonekana mlolongo wa magari. Natacha na marafiki zake walikuwa "tarehe 31" katika Baa hiyo. Walikuja kusherehekea hatua ya serikali ya kulegeza hatua za kuhibiti virusi vya Corona kwenye baa hii ya kisasa huko Kigali: “Sasa naweza kufanya tafrija, kutembelea marafiki wangu, kwenda sehemu nyingi za starehe. Kwa hivyo tunafurahi kweli kuona sheria ya kutotoka nje imesogezwa nyuma ”, amesema .

Sekta ya burudani inafunguliwa hatua kwa hatu lakini chini ya masharti: wafanyakazi waliopewa chanjo, vipimo vya haraka wakati mwingine vinahitajika kwenye mlango, idadi ndogo ya wateja pia ni lazima... Eugène Habimana, mmiliki wa baa ya kisasa ya Coco Bean, anatumai kuwa biashara itaanza haraka: “Tulipoteza mengi… tuna matatizo ya benki, kuna madeni mabaya, yote hayo. Kwa kila mtu Tutajaribu. Katika miezi mitatu, miezi miwili au mwezimmoja - sijui - itakuja na tutaanza tena maisha ya kawaida. "

Huko Kigali, zaidi ya 90% ya watu wazima tayari wamepewa chanjo, kulingana na mamlaka. Kampeni mpya ya chanjo imezinduliwa tu katika nchi nzima. Rwanda inatarajia kufikia kiwango cha chanjo ya 60% ifikapo mwisho wa 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.