Pata taarifa kuu
RWANDA

COVID-19: Serikali ya Rwanda yazindua tena kampeni ya chanjo

Rwanda inajaribu kudhibiti mlipuko wa tatu wa gonjwa la Covid-19. Katika wiki za hivi karibuni, nchi hiyo imerekodi kati ya kesi 500 na 1,000 za kila siku, takwimu ambazo hazijawahi kufikiwa. Hii ilisababisha serikali kutangaza katikati ya mwezi Julai marufuku kwa mara ya tatu ya watu kutotembea tangu kuzuka kwa janga hilo nchi humo.

Nchini Rwanda, malengo ya chanjo bado hayajafikiwa.
Nchini Rwanda, malengo ya chanjo bado hayajafikiwa. Ludovic MARIN AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Rwanda ilitangaza kwamba marufuku hiyo itadumu wiki mbili, wakati katika mji wa Kigali na katika wilaya zingine nane husika marufuku hiyo imeondolewa, na shule zimetakiwa kuanza shughuli zao.

Lengo ni kuchanja watu 350,000 kwa wiki sita. Serikali inataka kuokoa muda iliyopoteza na kufikia lengo lake la 30% ya Wanyarwanda ambao watakuwa wamepewa chanjo hadi mwishoni mwa mwaka huu. Wakati mwezi Machi, Rwanda ilikuwa kati ya nchi za kwanza kuanza kampeni yake ya chanjo na kupokea dozi kutoka mpango wa kimataifa wa ugawaji chanjo kwa nchi masikini wa COVAX. Miezi sita baadaye, Warwanda 460,000 pekee, au zaidi ya 3% tu ya raia wa Rwanda, ndio wamepokea dozi mbili za chanjo.

Lakini serikali iliweza kununua dozi zaidi ya milioni tatu hivi karibuni ya chanjo ya Pfizer / BioNTech, chanzo katika Wizara ya Afya kimebaini. Dozi hizo zitatolewa hatuakwa hatua, kampeni hiyo itaanza Jumanne wiki hii huko Kigali kisha nchini kote kwa raia wenye umri wa miaka 40 na zaidi.

Wakati huo huo, viongozi wamepunguza nusu ya bei ya vipimo vya haraka vya antijeni, ambavyo vitashuka kutoka karibu euro 10 hadi 5 kwa siku chache zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.