Pata taarifa kuu
KENYA

Kenya yapiga marufu raia wake kwenda kufanya kazi za ndani Saudi Arabia

Wakenya wapatao 89 wamepoteza maisha nchini Saudi Arabia katika kipindi cha miaka miwili iliyopita katika mazingira ya kutatanisha, hatua ambayo imesababisha serikali nchini Kenya kusitisha kwa muda raia wake wanaokwenda kufanya kazi za ndani kwenda katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Imebainika kuwa tangu kuanza kwa mwaka huu, wakenya 41 wamepoteza maisha nchini Saudi Arabia na kutambuliwa na serikali jijini Riyadh.
Imebainika kuwa tangu kuanza kwa mwaka huu, wakenya 41 wamepoteza maisha nchini Saudi Arabia na kutambuliwa na serikali jijini Riyadh. REUTERS - NJERI MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Wiki iliyopita, Katibu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Macharia Kamau, aliwaambia wabunge jijini Naiorbi kuwa, serikali ya Saudi Arabia inasema wakenya hao walipoteza maisha kwa sababu ya matatizo ya moyo.

Hata hivyo hivyo sababu za vifo hivyo zinaendelea kuzua mashaka hata kwa maafisa wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje nchini Kenya, kuwa raia wake walipoteza maisha kwa sababu ya matatizo ya moyo.

Imebainika kuwa tangu kuanza kwa mwaka huu, wakenya 41 wamepoteza maisha nchini Saudi Arabia na kutambuliwa na serikali jijini Riyadh.

Mwaka 2015 serikali ya Kenya ilitia saini mkataba na serikali ya Saudi Arabia kutambua mawakala ambao wanaowasaidia raia wa Kenya wanaotaka kwenda kufanya kazi za ndani kwenda nchini humo, lakini kwanza kuwasilisha mikataba ya Wakenya hao kwenye Wizara ya Kazi.

Hata hivyo, Mawakala wengi nchini humo hawajasajiliwa na serikali ya Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.