Pata taarifa kuu
KENYA

Kenya yakabiliana vilivyo na uwindaji haramu

Kenya inasema imefanikiwa pakubwa katika vita dhidi ya uwindaji haramu. Kwa miaka kadhaa wanyamapori wa Kenya wamepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na uwindaji haramu na muingiliano wa watu na wanyama hali ambayo imechangia kupotea kwa makazi ya wanyama hao na njia wanazotumia wakati wa kuhama.

Faru aliyeuawa na wawindaji haramu katika Hifadhi ya Lewa, Kenya, Novemba 2013.
Faru aliyeuawa na wawindaji haramu katika Hifadhi ya Lewa, Kenya, Novemba 2013. AFP PHOTO/ LEWA CONSERVANCY
Matangazo ya kibiashara

Hii inakuja wakati huu, ikitangaza sense au idadi ya wanyamapori nchini humo.

Kenya sasa ina ndovu 36,280 ikiwa ni ongezeko la asilimlia 12 kutoka idadi iliyokuwepo mwaka 2014.

Rais Uhuru Kenyatta amesema ni muhimu kwa idadi hiyo kufahamika.

Kenya ni ya nne duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya ndovu duniani baada ya Zimbabwe, Bostwana na Tanzania.

Lakini Shirika la Huduma kwa Wanyamapori nchini Kenya (KWS) linasema sensa, iliyofanywa kati ya mwezi Mei na Julai, ilionesha kupungua kwa idadi ya tembo, vifaru na spishi zingine za wanyama wanaokabiliwa na tishio la kuangamia.

Kulingana na KWS, Kenya ina vifaru 1,739, miongoni mwao vifaru weupe wa kaskazini duniani, vifaru weusi 897 na vifaru 840 weupe wa kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.