Pata taarifa kuu
KENYA-POMBE-AFYA

Kenya: Utata wa kisheria kuhusu pombe ya Mbangara pwani ya Kenya

Nchini Kenya, tunaendelea na ripoti zetu kuhusu pombe ya mbangara katika Kaunti ya Taita Taveta iliyoko Pwani ya nchi hiyo, lakini kumekuwa na mjadala kuhusu kupitishwa kwa sharia inayoruhusu kutenegzwa kwa pombe hiyo.

Pombe aina ya kisasa ya Heineken
Pombe aina ya kisasa ya Heineken Patrick HERTZOG AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Katika vikundi vikundi vidogo,Watu wanaendela kufurahia pombe.Wengi wakionekana kuunga mkono sheria  hiyo  kupitishwa  ili wasiinywe tena kisiri. 

“ Kwa nini wanatuambia tusinywe hii tunywe hii,pombe ni pombe,”mmoja wa walevi anasikika akisema. 

Wenzake wanajibu  kwa haraka, “ Ni kama tunapata juice,nikiamka asubuhi niko alive .” 

“ Eti mbangara mbangara ,kwani ina nini , kama ni kodi tutatoa ,na tujengewe ukumbi kabisa wa kuuziwa mbangara,” alisema mwingine 

Wauzaji vilevile wanataka ihalalishwe ili biashara yao iendelee kama kawaida. 

“ Siona ubaya wake ,ni vile tu haijahalalishwa,ikihalalisha hata ndo serikali sasa itaweka taratibu na masharti,”alisema Jimmy mmoja wa wagema kutoka Wesu. 

Naye Andrew Mangi anayeuzia pombe yake porini ili kuwakwepa polisi ,akaongeza, “ Kifedha wanatunyanyasa,ukikutwa na mtungi wa lita kumi ,tayari ni elfu kumi au upelekwe Manyani jela,wakitufunguliwa ,tuko tayari kupata leseni mradi tuambiwe ni ngapi.” 

Hata hivyo Bunge hilo limekanusha kuwepo kwa sheria  kama hiyo .Meshack Mghanga ni spika wa Bunge hilo. 

“ Kwanza kabla kuruhusu pendekezo la sheria ,jambo la kwanza,lazima liambatane na vipengele vya katiba  na lazima iwe sheria inayounga mkono maendelea,”alisema spika Meshak Mghanga. 

Mwenyekiti wa kamati ya biashara katika Bunge hilo Omari Nguzo anasema  mswada huo uliahirishwa ili mbunge Christopher Mwambingu aliyependekeza sheria hiyo ashauriane na kamati kwa kina. 

Na je shirika la kupambana na matumizi mabaya ya dawa za kulevya na vileo NACADA ,ina mtazamo gani kuhusu bunge kuwa na sheria kama hizo, 

Daniel Konyango ni mshauri wa kisheria, NACADA. 

“ Sheria ambazo haziambatani na sera za serikali kuu ,ni sheria ambayo haikubaliki,”alisema Konyango. 

Mawakili pia wana mtazamo  wao kuhusu mswada  kama huu. Steve Musili ni mmoja wao. 

“ Sheria yoyote ambayo haiambatani na katiba ya Kenya ,itaharamishwa na mahakama,”alisema wakili Steve. 

Bunge la Senate nchini lina jukumu kufuatilia utendakazi wa serikali za kaunti . Je inachukuliaje utata huu wa sharia ? 

Enock Wambua ni seneta wa kaunti ya Kitui eneo la mashariki. 

“ Tuko na jukumu la kuhakikisha kuwa sheria zinatengenezwa na kaunti zetu ,hazigongani na sheria za serikali kuu,” alisema Seneta Wambua. 

Iwapo  bunge hilo litazingatia hali halisi au sauti ya wafanyi biashara wa Mbangara  pamoja na wapenzi wa pombe  hiyo, wanaotaka ikubaliwe, ili   kupunguza  biashara haramu  , ni jambo la kusubiriwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.