Pata taarifa kuu
RWANDA-HAKI

Rwanda: Uamuzi wa kesi ya Paul Rusesabagina kutolewa Septemba 20

Uamuzi katika kesi ya Paul Rusesabagina, anayeelezwa kuwa shujaa katika filamu ya mwaka 2004 ya Hollywood ya Hotel Rwanda kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda umesogezwa mbele.

Paul Rusesabagina alipowasili katika mahakama ya Kigali mnamo Oktoba 2, 2020.
Paul Rusesabagina alipowasili katika mahakama ya Kigali mnamo Oktoba 2, 2020. Simon Wohlfahrt AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Paul Rusesabagina anayejulikana kwa kuokoa maisha ya watu elfu moja wakati wa mauaji ya kimbari ya Watutsi mnamo 1994, aliondoka nchini Rwanda kabla ya kuwa mpinzani na mkosoaji mkuu wa rais Paul Kagame.

Mwaka mmoja uliopita, alikamatwa, na kutekwa nyara kulingana na familia yake, na kurudishwa Kigali ambako tangu wakati huo anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi. Hukumu iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu ambayo ilipangwa kutolewa Alhamisi, Agosti 19, imeahirishwa hadi Septemba 20.

Hukumu ya kesi hiyo iliahirishwa kwa mwezi mmoja kwa sababu ya ukubwa wa kesi hiyo, mahakama ya Rwanda imesema. Uamuzi wa mahakama utacheleweshwa kwa mwezi mmoja kabla ya kujuwa hatima ya Paul Rusesabagina, ambaye anakabiliwa na kifungo cha maisha, na washtakiwa wenzake 20. Wote wanashukiwa kunwa katika kundi la FLN, kundi lenye silaha ambalo lilidai kuhusika na mashambulio kusini mwa Rwanda mnamo 2018. Kundi hlo linachukuliwa kama tawi la kijeshi la MRCD, vuguvugu la upinzani la Paul Rusesabagina.

Tangu kuanza kwa kesi hii ya muda mrefu, familia ya Paul Rusesabagina inalaani kuingiliwa kwa mahakama na serikali na kutaka aachiliwe. Ubelgiji na Bunge la Ulaya pia wameelezea wasiwasi wao juu ya mazingira ya kukamatwa kwake na jinsi kesi hiyo inavyoshughulikiwa.

Sio kesi ya haki, kulingana na Rusesabagina

Paul Rusesabagina, alikanusha kuhusika kwake katika mashambulio yaliyoua watu kadhaa nchini Rwanda, kulingana na mamlaka.

Mnamo Machi, alikataa kuripoti mahakamani, akibaini kwamba hatapata haki kati kesi hiyo. Kwa miezi kadhaa, mawakili wake wamehakikisha kwamba mamlaka ya Rwanda inazuia upande wa utetezi kumletea mteja wao nyaraka zinazohusu utaratibu wa kesi hiyo.

Hivi karibuni rais wa Rwanda Paul Kagame alisema anataka kuona haki inatendeka katika kesi ya Paul Rusesabagina.

Katika mahojiano na France 24, rais alionya vitendo vya ”kibaguzi” dhidi ya mifumo ya kimahakama.

" Nataka kushuhudia mwenyewe haki katika kesi hiyo. Kwanini unafikiria haki ni ya Ulaya au Marekani au kwa mwingine yeyote lakini sio sisi?", alisema rais Paul Kagame katika mahojiano na France 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.