Pata taarifa kuu
SALVA KIIR-SUDAN KUSINI

Salva Kiir na safari ya uongozi wa Sudan Kusini

Mpiganaji wa msituni ambaye sasa ni rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir aliongoza taifa lake kupata uhuru miaka 10 iliyopita na kumaliza miaka zaidi ya 20 ya kupigania kujitawala kutoka kwa serikali ya Sudan.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir AFP
Matangazo ya kibiashara

Muumini huyo wa dhehebu la Kanisa Katoliki, anafahamika sana kwa kutoa mahubiri katika Kanisa Kuu jijini Juba.

Anapenda kuvalia kofia nyeusi, aliyopewa zawadi kutoka kwa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani George Bush.

Kiir aliyejaliwa urefu wa kimo na ndevu, alifahamika sana kwa kuongoza vikosi vya wapiganaji msituni, badala ya kutoa hotuba za kisiasa.

Alipigana msituni wakati wa vita vya kwanza vya Sudan vilivyoanza punde baada ya Uhuru kutoka Uingereza kati ya mwaka 1956 hadi 1972, na baadaye kati ya 1983-2005, kudai Uhuru wa nchi yake Sudan Kusini.

Hata hivyo, alichukua hatamu za uongozi la kundi lililokuwa linapigania uhuru wa nchi yake mwaka 2005 baada ya kifo cha kiongozi wake na mpiganaji wa siku nyingi John Garang, aliyefariki dunia kufuatia ajali ya helikopta.

Upinzani wake wa kisiasa na Makamu wake wa rais Riek Machar ulizua vita vipya katika taifa hilo changa duniani.

Tangu mwaka 2013 mapigano hayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 400,000 na visa vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu kama ubakaji wa wasichana na wanawake pamoja na mateso yakishuhudiwa.

Mzaliwa wa jimbo la Warrap mwaka 1951, kutoka kabila la Dinka lenye watu wengi nchini Sudan Kusini, alitumia muda mrefu wa maisha yake akibeba bastola.

Punde tu, baada ya uhuru wa Sudan Kusini, taifa hilo chini ya Kiir, lilipata uungwaji mkono wa Jumuiya ya Kimaifa na kupata msaada wa Mabilioni ya Dola kuunga mkono miradi ya maendeleo.

Uongozi wake wa serikali baada ya miaka 10 ya uhuru, nchi hiyo imetawaliwa na ufisadi na mdororo wa uchumi.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa mwaka 2016 ilimshtumu yeyé na Makamu wake Machar kwa kuhusika na machafuko yaliyoendelea kutokea nchini humo.

Aidha, Kiir ameripotiwa kujilimbikizia mali za umma  na kuwekeza kwa kiasi kikubwa nje ya nchi huku wananchi wake wakiangamia kwa baa la njaa na umasikini.

Shirika la Kimataifa la utatuzi wa migogoro ICG linasema, rais Kiir anasalia kuwa kiongozi asiyetabirika, anayeongoza serikali isiyo imara na mpinzani wake Machar.

Anaelezwa kuwa mtu anayesikiliza zaidi kuliko kuongea na mara nyingi huwashangaza hata washauri wake kwa kubadilisha misimamo.

Wakati mwingine, anaelezwa kama kiongozi anayeweza kuliunganisha taifa lakini wakati mwingine, anayeweza kuligawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.