Pata taarifa kuu
RIEK MACHAR-SUDAN KUSINI

Riek Machar, kiongozi wa waasi mwenye historia ya vita nchini Sudan Kusini

Riek Machar ni kiongozi wa kundi la waasi ambaye ndani ya miaka 10 sasa, amekuwa ndani na nje ya serikali mara kadhaa.

Riek Machar Makamu wa kwanza wa Sudan Kusini
Riek Machar Makamu wa kwanza wa Sudan Kusini Akuot Chol AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Katika mzozo wa nchi hiyo, amesalia kuwa kiungo muhimu. Licha ya tabasamu lake la mara kwa mara, wanaomfahamu wanasema ana hasira na ni mkatili.

Alizaliwa mwaka 1953 katika jimbo la Unity. Kabila lake ni Nuer, jamii ya wafugaji nchini Sudan Kusini.

Kabila lake ndilo la pili kwa watu wengi nchini Sudan Kusini  baada ya lile la Dinka.

Hakupitia utamaduni ya kuchanjwa kwenye paja la uso, kuonesha utofauti ya wavulana na wanaume wa Nuer, lakini alipata nafasi ya kwenda Shule badala ya kuchunga mifugo.

Baada ya kusomea uhandisi katika Chuo Kikuu cha Khartoum, alipata shahada yake ya Udaktari kutoka chuo kikuu cha Bradford nchini Uingereza.

Mwaka 1983, alirejea Sudan na kujiunga kwenye vita kati ya Sudan Kaskazini na Kusini na kupata uugwaji mkono wa Wanuer wenzake, waliomwamini anaweza kutoa uongozi kwenye kundi la waasi ambalo lilikuwa linaongozwa na wale kutoka kabila la Dinka.

Hata hivyo, alichukizwa na jaribio la kiongozi la kundi la waasi wakati huo John Garang, kujaribu kumwondoa kama mmoja wa Makamanda wa kundi hilo,  yeyé pamoja na wenzake, akiwemo rais wa sasa Salva Kiir mwaka 1991.

Mapigano ya kikabila

Wakati kundi la waasi, lilipoendelea kugawanyika kwa misingi ya kikabila, Machar alishtumiwa kupanga mauaji dhidi ya waasi kutoka kabila la Dinka katika mji wa Bor mwaka 1991, katika mauaji ambayo yanasalia kuwa makubwa katika historia ya vita nchini humo.

Hii ilizua ulipizaji wa kisasi kati ya makundi ya makabila hayo mawili, yaliyokuwa yameoana na kushirikiana katika mambo mengi ya kijamii.

Machar baadaye aliondoa kwenye kundi kuu la waasi na kusaini mkataba na maadui wake wa zamani, serikali ya Khartoum.

Kurejea vitani 

Machar alirejea kwenye uwanja wa mapambano mwaka 2002. Baada ya mkataba wa amani kutiwa saini kati ya serikali ya Khartoum na waasi Kusini mwa nchi hiyo mwaka 2005, aliteuliwa kuwa Makamu rais wa eneo la Sudan Kusini.

Hii ni nafasi aliyoendelea kuishika hata baada ya Sudan Kusini kupata uhuru wake mwaka 2011, huku Salva Kiir akiwa rais.

Baada ya kujitenga na Sudan, nchi hiyo mpya ilianza kushuhudia changamoto za kiuchumi. Wananchi wengi waliishi kwa taabu. Changamoto hizo, zilimsukuma atangaze kuwania urais mwaka 2015.

Hali hiyo ilisababisha sintofahamu katika serikali ya Kiir ambaye aliamua kumfuta kazi Machar na washirika wake.

Vita vilizuka nchini humo na Machar akalazimika kuikimbia nchi.Aliwahi kuishi nchini Afrika Kusini na Ethiopia kwa nyakati tofauti.

Mwaka 2020, baada ya mkataba wa amani na rais Kiir mwaka 2018 aliapishwa kuwa Makamu wa rais kwa mara ya tatu.

Machar amemwoa, Angelina Teny ambaye sasa ni Waziri wa Ulinzi. Wana watoto kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.