Pata taarifa kuu

Sudani Kusini: Miaka 10, vita, njaa vyalisumbua taifa jipya duniani

Msikilizaji wakati huu taifa la Sudan Kusini, Ijumaa ya wiki hii likitarajiwa kusherehekea miaka 10 tangu lipate uhuru kutoka kwa Sudan, linaendelea kushuhudia hali mbaya ya umasikini iliyochangiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya maelfu ya raia.

Vikosi vya Ulinzi vya Sudan Kusini, lililokuwa likijulikana kama Jeshi la Ukombozi la watu wa Sudan, wakati wa mazoezi karibu na Juba, Aprili 26, 2019.
Vikosi vya Ulinzi vya Sudan Kusini, lililokuwa likijulikana kama Jeshi la Ukombozi la watu wa Sudan, wakati wa mazoezi karibu na Juba, Aprili 26, 2019. REUTERS/Andreea Campeanu
Matangazo ya kibiashara

Sudan Kusini, ilipata uhuru Wake kutoka kwa Sudan Julai 9 mwaka 2011 baada ya kura ya maoni iliyoshuhudia asilimia 99 ya raia wakiunga mkono taifa hilo kujitenga.

Β 

Mwaka 2005, mkataba wa amani ulitiwa saini kati ya serikali na waasi wa Sudan Kusini, ambapo ulitoa miaka sita ya Γͺneo hilo kujitawala kabla ya kujitenga rasmi, ambapo Salva Kiir aliapishwa kama rais na Riek Machar kama naibu Wake.

Β 

Kiir na Machar, walikuwa pamoja katika kudai uhuru kabla ya mwaka 2013 kutofautiana na kuingia katika vita, vilivyoshuhudia raia wakibakwa na wengine kuuawa.

Β 

Chini ya mkataba wa mwaka 2015, Machar alitejeshwa katika nafasi yake lakini punde tu yakazuka mapigano mengine hadi mwaka 2108 ambapo walikutanishwa na kutia saini mkataba wa amani ulipo sasa.

Β 

Kwa mujibu wa umoja wa Mataifa, mtu mmoja kati ya watani nchini humo anaishi katika hali ya umasikini, huku zaidi ya asilimia 60 wakikabiliwa na baa la njaa.

Β 

Sudan Kusini ambayo inategemea mapato yanayotokana na biashara ya mafuta, bado inakabiliwa na umasikini na vitendo vya rushwa, ambapo tangu mwaka 2018, mapato yake yalishuka maradufu.

Β 

Hata hivyo Sudan Kusini ni moja ya mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki yenye vivutio vingi kama mbuga za wanyama na maeneo anuai mengi na yenye rutuba, ikitajwa kama moja ya mataifa yenye idade kubwa ya ndege na maeneo oevu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.