Pata taarifa kuu
MAREKANI-TANZANIA

Marekani kushirikiana na Tanzania kupambana na Covid 19

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan siku ya  Jumanne alifanya  mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani  Anthony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken Kenzo Tribouillard POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yaliyojikita zaidi kwenye ushirikiano wa nchi hizo mbili  kupambana na  maambukizi ya  Covid-19.

Wiki iliyopita, rais Samia alidokeza kuwa nchi hiyo ina wagonjwa wa corona katika wimbi la tatu la maambukizi hayo na kutoa wito kwa wananchi wa taifa hiyo kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga.

Katika mtandao wake wa Twitter, Blinken amesifu jitihada za kiongozi huyo wa Tanzania kwa kufungua ukurasa mpya katika makabiliano ya janga la Corona.

Marekani imeahidi, kuisadia Tanzania katika mapambano hayo. Mazungumzo hayo pia yaligusia kuhusu namna ya  kuimarisha demokrasia kwa kuheshimu haki za kisiasa, za mashirika ya kiraia na uhuru wa vyombo vya Habari.

Aidha, viongozi hao wawili wamejadiliana kuhusu masuala ya usalama na mchango wa Tanzania kutuma wanajeshi wa kulinda amani hasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.