Pata taarifa kuu
RWANDA - SIASA

Rwanda - Jean-Claude Iyamuremye mshukiwa wa mauwaji ya kimbari afungwa jela miaka 25

Mshukiwa wa mauwaji ya kimbari ya mwaka 1994, nchini Rwanda,  Jean-Claude Iyamuremye, amehukumiwa kifungo cha miaka 25, baada ya kupatikana na hatia ya kuwa mwanachama kundi la watu wenye silaha waliotekeleza mauwaji ya raia zaidi ya 800,000, akiwa na umri wa miaka 19

Jean-Claude Iyamuremye mshukiwa wa mauwaji ya kimbari nchini Rwanda
Jean-Claude Iyamuremye mshukiwa wa mauwaji ya kimbari nchini Rwanda © courtesy
Matangazo ya kibiashara

Katika kesi yake ambayo imechukuwa muda wa miaka 5 Iyamuremye, amekuanusha kuhusika na mauwaji ya raia wa Kitutsi, akijitetea kuwa mamake mzazi alikuwa Tutsi.

Jaji aliyekuwa anaskiza kesi hiyo amesema angetoa hukumu ya Iyamuremye, kufungwa kifungo cha maisha, ila amemsamehe kwani wakati wa mauwaji hayo alikuwa mdogo na alisadia baadhi ya familia za Tutsi.

Iyamuremye alikamatwa mwaka 2013, nchini Uholanzi, alikokuwa anafanya kazi kama dereva katika balozi za Isreali na Finland.

Serikali ya Uholanzi ilimrejesha Iyamuremye, nchini Rwanda mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.