Pata taarifa kuu
EAC-UCHUMI

Baadhi ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zawasiisha bajeti zao

Mawaziri wa fedha kutoka mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wamekuwa wakiwasilisha bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwenye mabunge yao.

Mji wa Arusha, makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Mji wa Arusha, makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Mkataba uliounda Jumuiya ya Afrika Mashariki unataka mataifa yote ya Jumuiya hiyo kuwasilisha bajeti zao kwa siku moja.

Hata hivyo, mataifa anzilishi ya Jumuiya hiyo, Kenya, Uganda na Tanzania ndio yaliyowasilisha bajeti zao leo.

Nchini Kenya, Waziri wa fedha  Ukur Yatani  amewasilisha bajeti ya Dola Bilioni 33.3 wakati huu nchi hiyo ikikabiliwa na kipindi kigumu kiuchumi kufuatia janga la Covid 19.

Nchini Tanzania, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amesema wakati huu, deni ya serikali nchini humo linakifikia fedha za nchi hiyo Trilioni 60.9.

Nchini Uganda, Waziri wa Fedha Amos Lugoloobi, amewasilisha Bajeti ya Dola Bilioni 12.61 ambayo amesema itasaidia kuimarisha maisha ya wananchi wa taifa hilo.

Rwanda haikutoa sababu ya kuchelewesha usomaji wa bajeti ya nchi hiyo, huku Burundi na Sudan Kusini ambazo mwaka wao wa fedha huanza mwezi Januari, wakiendelea kupewa muda kuanza kusoma bajeti zao mwezi Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.