Qatar: Mkenya Malcolm Bidali azuiliwa kwa wiki tatu bila mashtaka yoyote
Malcolm Bidali, raia wa Kenya, amezuiliwa nchini Qatar kwa wiki tatu na mashtaka dhidi yake bado hayajulikani. Mlinzi huyo amekuwa akiandika, kwa jina bandia, juu ya hatima ya wafanyakazi wahamiaji nchini humo.
Imechapishwa:
"Anazuiliwa kwa usiku wa ishirini bila mashitaka yoyote". Kwenye ukurasa wake wa twitter, Vani Saraswathi amekuwa akihesabu idadi ya siku tangu Malcolm Bidali akamatwe. Ni mhariri mkuu na mkurugenzi wa mradi wa Migrant-Rights, shirika la haki za wahamiaji lililoko katika nchi za Ghuba. Ni kwenye wavuti huo Mkenya huyo aliandika kwa jina bandia la "Noah".
20 nights detained without charges. @noaharticulates’s mum says he is being held for 23 hours in solitary.
— Vani Saraswathi (@vanish_forever) May 24, 2021
Qatar Constitution says “…no person may be subjected to torture, or any degrading treatment; and torture shall be considered a crime punishable by law.”#WhereIsMalcolm
Katika kilele cha tukio hilo, Malcolm Bidali alifafanua maisha yake ya kila siku kama mlinzi huko Qatar. Ushuhuda adimu, ulioandikwa kwa mtu wa kwanza, ambaye anaweza kuwa chanzo cha kukamatwa kwake, mashirika makubwa yanayotetea haki za binadamu yamesema.
Kwa kweli, sababu hasa ya kukamatwa kwake bado haijulikani. Kijana huyo wa miaka 28 "anachunguzwa kwa kukiuka sheria na kanuni za usalama," mamlaka ya Qatar imesema.
Wakati Kombe la soka la Dunia la mwaka 2022 linakaribia, mambo ya Bidali bado ni mwiba mwingine kwa Qatar. Kwa miezi kadhaa, kampeni ya kususia michano hiyo ya kimataifa imeshutumu jinsi wafanyakazi wahamiaji wanavyofanyiwa madhila nchini humo.