Pata taarifa kuu
KENYA

IMF yaidhinisha msaada wa dola bilioni 2.34 kwa Kenya

Bodi ya wakurugenzi ya shirika la Fedha la kimataifa, IMF, limedhinisha msaada wa dola bilioni 2.34 kwa Kenya "ili kushughulikia mahitaji ya haraka ya kupunguza udhaifu wa deni," taasisi hiyo imesema katika taarifa.

Nembo ya shirka la Fedha la kimataifa, IMF.
Nembo ya shirka la Fedha la kimataifa, IMF. AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linabainisha kuwa msaada huu umetolewa katika mfumo mpana ulio rahisi wa Mikopo (ECF) na mfumo mpana wa fedha (EFF).

Msaada huo utatolewa kwa kipindi cha miezi 38 au zaidi ya miaka mitatu. Kiasi cha malipo ya haraka ni takriban dola milioni 307.5, inayoweza kutumika kwa msaada wa bajeti kwa ajili ya kusaidia kupunguza umaskini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.