Pata taarifa kuu
BURUNDI

Sera ya rais wa Burundi dhidi ya ufisadi yazua utata

Evariste Ndayishimiye, rais wa Burundi tangu Juni 20, 2020, ameweka vita dhidi ya ufisadi kuwa moja ya vipaumbele vyake katika nchi iliyoorodheshwa kati ya nchi 10 za kwanza zilizokithiri kwa kulingana na shirika la kimataifa la Amnesty International.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye AFP Photos/Tchandrou Nitanga
Matangazo ya kibiashara

Miezi tisa akiwa uongozini matamshi ya Bw Ndayishimiye ya hivi karibuni kuhusu sera yake dhidi ya ufisadi yamezua utata.

Evariste Ndayishimiye alisikika akisema kwamba swala lililopo sio kuanza kuendesha uchunguzi dhidi ya waliohusika na uporaji wa mali ya umma, vinginevyo itachukuwa muda mrefu katika uchunguzi sababu uporaji huu umeanza tangu kipindi cha ukoloni.

 Badala yake amesema wahusika wa ubadhirifu wa mali ya umma tangu pale alipokabidhiwa hatamu ya nchi ndio ambao watafunguliwa mashtaka.

 Kauli hii imekosolewa vikali na mkuu wa shirika linalohusika na kupiga vita rushwa nchini Burundi OLUCOME ambapo kiongozi wake Gabriel Rufyiri amesema sheria kuhusu kupiga vita rushwa ipo tangu mwaka 2006 chini ya utawala wa chama cha CNDD-FDD, na kwamba ameshtushwa na kauli hiyo ya rais, ambapo kwa sasa nchini Burundi swala la rushwa « limehalalishwa ».

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.