Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Joe Biden akaribisha uhusiano usiovunjika kati ya Washington na London

Joe Biden anazuru Uingereza Jumatatu hii, Julai 10. Rais wa Marekani aliwasili jana usiku mjini London, ambako atatua kabla ya kwenda Vilnius kwa mkutano wa kilele wa NATO Jumanne na Jumatano. Rais Joe Biden alikwenda asubuhi Downing Street, kukutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu Rishi Sunak.

Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak katika 10 Downing Street London, Jumatatu Julai 10, 2023.
Rais wa Marekani Joe Biden wakati wa mkutano wake na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak katika 10 Downing Street London, Jumatatu Julai 10, 2023. AP - Susan Walsh
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa London, Émeline Vin

Rishi Sunak ametoa zulia jekundu kwa Joe Biden nje ya makazi yake ya Downing Street. Wawili hao walitumia saa moja kwenye bustani, wakinywa chai.

Hakukuwa na mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa mazungumzo yao, lakini rais wa Marekani amethibitisha kwamba "hangeweza kukutana na rafiki wa karibu au mshirika mkubwa", na akahakikisha kwamba uhusiano kati ya nchi zao mbili uko "imara kama jiwe". Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Uingereza amesema ana uhakika kwamba London na Washington ni miongoni mwa washirika wa karibu ndani ya NATO. Huu ni mkutano wao wa sita ndani ya kipindi cha miezi saba.

Mtazamo tofauti

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa leo asubuhi, ushirikiano wa kiuchumi na usalama, katika mtazamo tofauti. Wiki iliyopita, Uingereza ilipinga uamuzi wa Marekani wa kupeleka mabomu ya tata nchini Ukraine.

Joe Biden pia alisafiri hadi Windsor, ambapo alikutana na Mfalme Charles, kwa mara ya kwanza tangu kukabidhiwa kiti ch ufalme.

Kwa kifupi jinsi ilivyo kuwa ziara ya Joe Biden huko London

Baada ya mkutano wa takriban dakika arobaini, rais wa Marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza walihakikisha katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba wanaendelea "kuunga mkono", pamoja, Ukraine na kwamba wanafahamu umuhimu wa kutoa silaha kwa Kiev ili kuhakikisha ushindi dhidi ya Moscow. Na bado, siku chache mapema, Rishi Sunak alikosoa usafirishaji wa Joe Biden wa mabomu tata kwenda Ukraine.

Katika Downing Street, wawili hao pia walijadili uanachama wa Sweden kujiunga na NATO - ambao wote wanaunga mkono - pamoja na ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia.

Akiwa ndani ya gari lake la kivita, Beast, Joe Biden alitumia alikwenda huko Windsor alaasiri. Rais na Mfalme Charles walionekana wakitabasamu. Wakati wa mkutano huu, mabadiliko ya hali ya hewa - mojawapo ya suala alilopenda zaidi - lilijadiliwa, mbele ya Waziri wa Mazingira wa Uingereza na mjumbe maalum wa Marekani kuhusu Tabia nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.