Pata taarifa kuu

Antonio Guterres anashutumu hatua ya ulimwengu kwa dharura ya tabia nchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasikitika kukosekana kwa hatua madhubuti za Mataifa kukabiliana na dharura ya tabia nchi na kuomba kupigwa marufuku kwa nishati ya mafuta.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari. AP - Hadi Mizban
Matangazo ya kibiashara

Maneno ya Antonio Guterres ni makali. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema siku ya Alhamisi, Juni 15 katika mkutano na waandishi wa habari kwamba mwitikio wa pamoja wa ulimwengu ni "wa kusikitisha" licha ya matarajio yaliyotangazwa ya janga la tabia nchi. Hasa, kwa mara nyingine tena ameshambulia nishati ya mafuta, ambayo anaona "hayaendani" na maisha ya ubinadamu.

"Tunakimbilia kwenye maafa, huku watu wengi swakiwa tayari kucheza kamari kila kitu kwa matamanio, teknolojia ambayo haijathibitishwa au marekebisho ya haraka," Antonio Guterres amesema katika taarifa yake. Sera za sasa zinaongoza ulimwengu kuelekea ongezeko la joto la +2.8°C kufikia mwisho wa karne hii. Hii inatangaza janga. Hata hivyo majibu ya pamoja ni ya kusikitisha. »

'Ni wakati wa kuamka na kuchukua hatua'

"Nchi ziko mbali na kutekeleza ahadi na walichojikubalisha kuhusiana na Tabia nchi. Ninaona ukosefu wa hatua. Kutokuaminiana. Ukosefu wa msaada. Ukosefu wa ushirikiano. Na shida nyingi za uwazi na uaminifu, "amesema Katibu Mkuu, ambaye ataandaa mkutano wa kilele juu ya hatua ya hali ya hewa huko New York mnamo Septemba 20.

"Ni wakati wa kuamka na kushika kasi," amesihi, bado anaamini kwamba kufikia lengo bora la makubaliano la kupunguza ongezeko la joto hadi +1.5°C "bado kunawezekana" . Lakini kwa hilo, lazima tuchukue hatua "mara moja", kuanzia "na moyo uliochafuliwa wa shida ya hali ya hewa: nishati ya mafuta. "

"Tatizo sio tu uzalishaji wa mafuta. Ni nishati ya mafuta yenyewe, sina la kuongeza. Viwanda katika sekta ya mafuta, makaa ya mawe, mafuta na gesi, ni lengo kuu la Katibu Mkuu, ambaye amewataka kuachana na "bidhaa isiyoendana na maisha ya binadamu", amebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.