Pata taarifa kuu

Waislamu waanza mfungo wa mwezi wa Ramadhan

Waislamu kote ulimwenguni wanaanza leo Alhamisi Machi 23 ibada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, wakati raia katika nchi mbalimbali hasa barani Afrika wanakabiliwa na ukosefu wa chakula, katika nchi mbalimbali bei ya chakula ikipanda kila kukicha, hususan barani Afrika.

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan waanza kwa Waislamu. Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa kusoma sana Q'uran.
Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan waanza kwa Waislamu. Mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa kusoma sana Q'uran. © SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mamilioni ya Waislamu duniani kote leo Alhamisi wameanza kufunga kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambapo hujizuiya kula na kunywa kuanzia alfajiri hadi jua linapozama takriban siku 30 au 29 kutegemea na muandamo wa mwezi.

Mwezi wa Ramadhani ni moja ya miezi mitukufu katika kalenda ya kiislamu ambayo husubiriwa kwa hamu kubwa na waumni wote wa kiislamu ulimwenguni.

Mwezi wa Ramdhani ni mwezi wa kuzidisha upendo, kutoa sadaka na kuwakumbuka wote wale wenye kuhitaji msaada.

Ramadhan huanza mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislam ambapo Waislam wanaamini Q'uran Takatifu iliwasilishwa kwa Mtume Mohammad katika karne ya saba mnamo mwezi wa Ramadhan.

Waislamu wanaamini kuwa huu ni mwezi wa kupatiwa msamaha na Mwenye-Enzi-Mungu kwa hiyo huzidisha ibada kwa wingi na kuwa karibu na Mwenye-Enzi-Mungu.

Saudi Arabia mahala kulikozaliwa Uislamu pamoja na nchi kadhaa za Mashariki ya Kati,Ghuba na nchi nyingi za Kiislam ikiwemo Indonesia taifa lenye idadi kubwa kabisa ya Waislamu duniani na Ulaya Waislamu wameanza kufunga leo alhamisi kutimiza nguzo ya tano ya Uislamu, mwezi ambao aya ya kwanza ya Q'uran iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW).

Ni wakati ambapo Waislamu hutafakari kwa undani kabisa matendo yao, kuwa wanyenyekevu zaidi kwa Mwenye-Enzi-Mungu kwa kufuata maamrisho yake na kuachana na maovu yote alilyoyakataza pamoja na kuweza kujizuiya na matamanio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.