Pata taarifa kuu

Mtumiaji wa mtandao agoma kula baada ya kuhukumiwa kwa 'kudhalilisha dini ya Kiislamu'

Nchini Morocco, mtumiaji wa mtandao wa Morocco amekuwa kwenye mgomo wa kula kwa karibu wiki mbili kupinga hukumu yake iliyotolewa katikati ya mwezi Septemba hadi miaka miwili jela kwa "kudhalilisha dini ya Kiislamu" kwenye Facebook, kulingana na familia yake.

Bi. Fatuma alifunguliwa mashitaka kwa kutoa maoni yake kwa sauti ya kejeli kwa Kiarabu kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusu aya za Qur'ani na hadithi za Mtume Muhammad, zinazochukuliwa kuwa takatifu katika utamaduni wa Kiislamu.
Bi. Fatuma alifunguliwa mashitaka kwa kutoa maoni yake kwa sauti ya kejeli kwa Kiarabu kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusu aya za Qur'ani na hadithi za Mtume Muhammad, zinazochukuliwa kuwa takatifu katika utamaduni wa Kiislamu. (Wikipedia)
Matangazo ya kibiashara

Fatima Karim, 39, "alianza mgomo wa kula siku 13 zilizopita ili kupinga hukumu yake kali," mwanafamilia mmoja ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne, ambaye aliomba jina lake lisitajwe. "Tunahofia kuzorota kwa hali yake ya afya."

Akiwa kizuizini tangu katikati ya mwezi wa Julai, Bi. Fatuma alifunguliwa mashitaka kwa kutoa maoni yake kwa sauti ya kejeli kwa Kiarabu kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusu aya za Qur'ani na hadithi za Mtume Muhammad, zinazochukuliwa kuwa takatifu katika utamaduni wa Kiislamu.

Mtumiaji wa mtandao wa Morocco alihukumiwa Agosti 15 hadi miaka miwili jela kwa "kushambulia dini ya Kiislamu kwa njia za kielektroniki" na mahakama ya mwanzo ya Oued Zem, mashariki mwa Casablanca. Uamuzi huo ulithibitishwa mnamo Septemba 14.

Mbele ya mahakama ya mwanzo, alidai haki yake ya uhuru wa kujieleza, unaohakikishwa na Katiba ya Morocco. Pia alikuwa ameomba msamaha hadharani kwa "mtu yeyote ambaye alihisi kukerwa" na machapisho yake, na kuhakikisha kwamba hakuwahi kudhalilisha Uislamu, dini ya serikali nchini Morocco.

Kesi hiyo ilianzishwa na upande wa mashtaka. Ibara ya 267-5 ya Sheria ya Makosa ya Jinai ya Morocco, ambapo Fatima Karim alihukumiwa, humuadhibu "mtu yeyote anayedharau dini ya Kiislamu" kwa miezi sita hadi miaka miwili jela.

Adhabu hiyo huenda ikaongezwa hadi miaka mitano jela ikiwa kosa hilo litakuwa limefanywa hadharani - "ikiwa ni pamoja na njia za kielektroniki". Watetezi wa haki za binadamu wanalaani Ibara hii ya sheria ambayo inazuia uhuru wa kujieleza na ambayo maneno yake "hayaelezi bayana ukweli ambao unaweza kuwa tusi au kejeli".

Kesi sawa na hiyo ilisababisha mwaka wa 2021 kuhukumiwa kwa mwanamke, raia wa Italia mwenye asili ya Morocco kifungo cha miaka mitatu na nusu kwa "kudhalilisha dini ya Kiislamu" baada ya kuchapisha sentensi za kejeli kwenye Facebook akiiga aya za Qur'ani. Mwanamke huyo aliachiliwa muda mfupi baadaye, kifungo chake kikiwa kilipunguzwa katika Mahakama ya Rufaa hadi kifungo cha miezi miwili gerezani, kufuatia kampeni ya maandamano ya watetezi wa haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.