Pata taarifa kuu
UGANDA-DINI-UISLAM

Polisi ya Uganda kujieleza kuhusu uvamizi dhidi ya Msikiti wa Nakasero

Jeshi la Polisi nchini Uganda, linatarajiwa kutoa maelezo hivi leo ni kwanini kikosi maalum cha kupambana na ugaidi kilivamia Msikiti wa Tabliq Nakasero jijini Kampala hapo jana na kuwakamata watu zaidi ya 10.

Olisi ya Uganda kujieleza kuhusu uvamizi iliyoufanya katika Msikit wa Tabliq Nakasero jijini Kampala.
Olisi ya Uganda kujieleza kuhusu uvamizi iliyoufanya katika Msikit wa Tabliq Nakasero jijini Kampala. Reuters/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Jumanne wiki hii, polisi walithibitisha uvamizi huo lakini wakakataa kutoa sababu ya hatua hiyo, hali ambayo imeendelea kuzua wasiwasi kwa waumini wa Kiislamu na wanaobudu katika Msikiti huo.

Awali Habib Buwembo mmoja wa wasemaji wa Msikiti huo alisema maafisa hao walivunja milango ya Ofisi ya Msikiti na kuchukua Kompyuta pamoja na stakabadhi muhimu.
Aidha, alisema walinzi 11 walikamatwa wakati wa msako huo na hawajulikani waliko.

Msemaji wa polisi Andrew Felix Kaweesi alithibitisha kufanyika kwa msako huo na kueleza kuwa maelezo ya kina yatatolewa katika siku zijazo.

Haijafahamika ikiwa msako huu, unahusishwa na kukamatwa kwa viongozi wakuu wa dhehebu la Kiislamu la Jamat Dawatil Salafiya.

Kumekuwa na hali ya wasiwasi katika Msikiti huo baada ya kukamatwa kwa viongozi wa dhehebu hilo akiwemo, Sheikh Yahya Mwanje na Katibu Mkuu Ayub Nyende miongoni mwa wengine.

Uganda imekuwa ikikabiliwa na mauaji ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu akiwemo Hassan Kirya, msemaji wa dhehebu la Kibuli, Amir wa zamani wa jiji la Kampala Mustafa Bahiga na Mhubiri wa Kishia Abdul Qadir Muwaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.