Pata taarifa kuu

Kiongozi wa Syria Bashar Al-Assad azuru Moscow kujadili maridhiano kati ya Uturuki na Syria

Rais wa Urusi Vladimir Putin amempokea kiongozi wa Syria Bashar Al-Assad mjini Moscow Jumatano Machi 16, wakati ambapo Ikulu ya Kremlin inaongeza juhudi zake za kupatanisha Uturuki na Syria na kusisitiza uzito wake wa kidiplomasia licha ya kutengwa kwake kufuatia uvamizi wake nchini Ukraine.

Kiongozi wa Syria Bashar al-Assad na Rais wa Urusi Vladimir Putin wakiwa katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Machi 15, 2023.
Kiongozi wa Syria Bashar al-Assad na Rais wa Urusi Vladimir Putin wakiwa katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Machi 15, 2023. © Sputnik/Vladimir Gerdo/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Juhudi hizi zinakuja wakati uhusiano wa kidiplomasia umeshika kasi Mashariki ya Kati baada ya kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Iran na Saudi Arabia chini ya mwamvuli wa Beijing. Kwa upande wa Kremlin, wanasema kuandaa maridhiano kati ya Uturuki na Syria, uliodorora tangu mwaka 2011, itakuwa kuonyesha uzito wa kidiplomasia wa Moscow licha ya kutengwa na nchi za Magharibi tangu mashambulizi yake nchini Ukraine.

Mkutano kati ya Vladimir Putin na Bashar Al-Assad ulianza mwendo wa saa mbili usiku, kulingana na picha zilizorushwa hewani kwenye televisheni ya Urusi. Mawaziri kadhaa walishiriki katika mkutano huu, ambao ulifuatiwa na mazungumzo kati ya viongozi hao wawili. "Tunawasiliana mara kwa mara na uhusiano wetu unaendelea," alisema Vladimir Putin mwanzoni mwa mazungumzo, akikaribisha "matokeo muhimu" yaliyopatikana na Moscow na Damascus katika "mapambano dhidi ya ugaidi wa kimataifa". Kwa upande wake, Bashar Al-Assad alieleza kuunga mkono mashambulizi ya kijeshi ya Moscow nchini Ukraine na kusema anatumai kuwa ziara yake itaashiria "hatua mpya katika uhusiano wa Syria na Urusi".

Kuelekea maridhiano ya Uturuki na Syria?

Lakini moja ya mada kuu kwenye ajenda ya mkutano huu ni mchakato wa maridhiano kati ya Ankara na Damascus, ambao Moscow inataka kuharakisha, hasa kwa kuandaa mkutano wa kilele na Bashar Al-Assad na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. "Uhusiano kati ya Uturuki na Syria hakika utafufuliwa kwa njia moja au nyingine" na majadiliano kati ya Vladimir Putin na Bashar Al-Assad, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema siku ya Jumatano.

Licha ya maslahi yao tofauti katika Syria na uanachama wa Uturuki kaika Jumuiya ta Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO, Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan wameshirikiana kwa karibu katika miaka ya hivi karibuni, hali ambayo inaelezea jukumu la Moscow katika jaribio la maridhiano kati ya Uturuki na Syria. Wanadiplomasia kutoka Urusi, Uturuki, Syria na Iran wanatarajiwa kukutana wiki hii mjini Moscow ili kuandaa mkutano kati ya mawaziri wao wa mambo ya nje, kabla ya uwezekano wa mkutano wa kilele wa marais.

Mwishoni mwa mwezi Desemba, Mawaziri wa Ulinzi wa Uturuki na Syria walikutana huko Moscow na mwenzao wa Urusi, ikiwa ni mara ya kwanza tangu 2011.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.