Pata taarifa kuu

Asili ya Uviko: WHO yaitaka Washington kupeana taarifa na kutoa ushahidi wake

Shirika la Afya Duniani, WHO, imetoa wito kwa nchi zote siku ya Ijumaa kushiriki habari zao juu ya asili ya Uviko, baada ya shirika la kijasusi la FBI na Wizara ya Nishati ya Marekani kubaini kwamba uvujaji wa maabara ulisababisha janga hilo.

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi.
Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi. © Denis Balibouse/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika siku za hivi karibuni, asili ya janga la Uviko-19 imesababisha kuongezeka kwa mvutano.

"Ikiwa nchi ina habari juu ya asili ya janga, ni muhimu kwamba WHO na jamii ya wanasayansi ya kimataifa vinashirikishwa kwa habari hii ," Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema wakati wa mkutano wake wa kila siku na waandishi wa habari.

Sio swali la "kutaja wahusika", amebaini, lakini "kuendeleza uelewa wetu juu ya jinsi janga hili lilianza, ili tuweze kuzuia milipuko na majanga ya baadaye, kujiandaa na kukabiliana na majanga hayo".

Mkurugenzi wa FBI Christopher Wray alisema wiki hii kwamba ajali ya maabara huko Wuhan nchini China "inawezekana" kuwa asili ya janga la Uviko-19, siku mbili baada ya nadharia kama hiyo iliyotolewa na Wizara ya Nishati ya Marekani.

Akihojiwa hasa juu ya mada hii, Maria van Kerkhove, anayehusika na majibu dhidi ya UViko katika Shirika la Afya Duniani, WHO, ameeleza kwamba shirika hilo liliomba habari kutoka kwa maafisa waandamizi wa uwakilishi Marekani katika Umoja wa Mataifa huko Geneva.

"Tumetuma maombi ya kupata habari juu ya ripoti ya mwisho katika wizara ya nishati, lakini pia juu ya ripoti mpya za mashirika tofauti ya Marekanj," alisema.

"Kwa sasa, hatuwezi kupata ripoti hizi au data ambazo zimefanya uwezekano wa kutoa ripoti hizi," amesema. Jumuiya ya wanasayansi inazingatia kuwa ni muhimu kujua asili ya janga hili ili kuweza kukabiliana nalo au hata kuzuia janga jipya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.