Pata taarifa kuu

Chanjo: Amnesty International yashutumu maabara kwa kupuuza nchi masikini

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limeshutumu maabara ya dawa ambayo yanatengeneza chanjo za Covid-19 kwa kuchochea "mgogoro wa haki za binadamu ambao haujawahi kutokea", ikitaka kutolewa dozi bilioni mbili kwa nchi masikini.

Dozi mbili za chanjo ya Pfizer na Moderna.
Dozi mbili za chanjo ya Pfizer na Moderna. REUTERS - Dado Ruvic
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti ya leo Jumatano iliyopewa jina "Dozi mbili pasipokuwepo na usawa: Maabara ya Dawa na mgogoro wa Chanjo ya Covid-19," shirika la Amnesty International linasema maabara nyingi haziweki kipaumbele kwa nchi masikini zaidi. Ripoti hii inakuja wakati mkutano wa kimataifa kuhusu chanjo umepangwa kufanyika Jumatano wiki hii. Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi kutangaza ahadi za ziada za kupatia chanjo nchi zilizoendelea.

Kutoa chanjo ykwa dunia ndiyo njia yetu pekee ya kuondokana na mgogoro huu. Hatua budi ya kukaribisha kampuni hizi, ambazo zilitengeneza chanjo hizi haraka sana, kama mashujaa, "Katibu Mkuu wa Amnesty Agnès Callamard amesema katika taarifa." Badala yake, kwa aibu yao na huzuni wetu kwa pamoja, kizuizi cha makusudi cha Big Pharma cha kuhamisha ujuzi wao kwa niaba ya mataifa tajiri kumesababisha upungufu wa chanjo ambayo ni ya kutabirika na ya kuumiza kwa nchini nyingi ”.

Kampuni hizi ziliamu kuuza chanjo kwa bei ya juu. Hii inamaanisha kuwa ni nchi tajiri tu ambazo zina uwezo wa kununua chanjo hizi. Pfizer na BioNTech hadi sasa wamewasilisha chanjo zaidi ya tisa kwa Sweden kuliko kwa nchi zote zenye kipato cha chini.

Amnesty International imekagua sera za AstraZeneca, Pfizer, BioNTech, Moderna, Johnson & Johnson na Novavax - na kubaini kwamba chanjo zao bado haijaidhinishwa - kulingana na haki za binadamu, bei, hati miliki, kugawana maarifa na teknolojia, ugawaji wa dozi na uwazi. Limehitimisha kuwa "kwa viwango tofauti, maabara sita za chanjo zimeshindwa kutekeleza majukumu yao kuhusiana na haki za binadamu." Kati ya dozi bilioni 5.76 zilizotolewa, 0.3% pekee zilitumwa katika nchi zenye kipato cha chini, 79% zilitumwa katika nchi za kipatocha kati na cha juu, Amnesty International imeongeza.

Faida ya mabilioni ya dola

Pfizer, BioNTech na Moderna wanapanga kupata faida ya dola bilioni 130 kufikia mwisho wa mwaka 2022, kulingana na shirika la Amnesty International, ambalolinabaini kwamba "faida haipaswi kuja kabla ya maisha." Wakati maabara mengi yamepokea "mabilioni ya dola kama ufadhili wa serikali, watengenezaji wa chanjo wamehodhi miliki, wamezuia uhamishaji wa teknolojia, na hatua kali ambazo zinaweza kupanua utengenezaji wa chanjo hizi ulimwenguni kote." Chanjo ", shirika hilo limeshtumu.

Amnesty International inatoa wito kwa kampuni na serikali "kubadilisha njia" ili kutoa chanjo bilioni mbili kwa nchi za kipato cha chini na cha kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.