Pata taarifa kuu
DRC

COVID-19: Marekani yatoa dozi 250,000 za chanjo ya Moderna kwa DRC

Serikali ya Marekani, kupitia mpango  wa COVAX, imetoa dozi 250,000 za chanjo ya Moderna kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika vita dhidi ya kuenea kwa virusi vya COVID-19.

Vipimo vipya vya Moderna vitawezesha zaidi ya watu 120,000 kupata chanjo kamili katika majimbo 15 yaliyotambuliwa na Mpango wa Chanjo (EPI), UNICEF inasema.
Vipimo vipya vya Moderna vitawezesha zaidi ya watu 120,000 kupata chanjo kamili katika majimbo 15 yaliyotambuliwa na Mpango wa Chanjo (EPI), UNICEF inasema. AFP - ARSENE MPIANA
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, ambalo limetoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na chanjo hiyo, limesema dozi hizo za chanjo ziliwasili katika mji mkuu wa DRC, Kishasa Jumatatu (Septemba 6).

Msaada huu wa Marekani unatoa nafasi ya ziada kwa chanjo salama na madhubuti, ikiwa ni pamoja na chanjo ya kwanza iliyopokelewa nchini hivi karibuni, na hivyo kuimarisha imani ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kampeni ya chanjo.

Wakati DRC ilipokea dozi za kwanza za chanjo mwezi Machi mwaka huu, taarifa hiyo imebainisha, rais wa Jamhuri, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, wakati huo alitangaza kwamba nataka chanjo mbalimbali kwa nchi yake kudhibiti janga la COVID-19.

Nchini DRC viwango vya chanjo viko chini sio tu dhidi ya COVID-19, lakini pia dhidi ya magonjwa mengine hatari, kama vile surua.

Vipimo vipya vya Moderna vitawezesha zaidi ya watu 120,000 kupata chanjo kamili katika majimbo 15 yaliyotambuliwa na Mpango wa Chanjo (EPI), UNICEF inasema.

Dawa hizo zitahifadhiwa jijini Kinshasa kabla ya kusafirishwa kwenda kwenye maeneo ya chanjo nchini.

“Maelfu ya Wacongo watachanjwa na kulindwa dhidi ya COVID-19 baada ya msaada huu kutoka kwa Serikali ya Marekani. Tuna uhakika kuwa chanjo hizi zitakubaliwa nchini DRC ambapo UNICEF na washirika wake wanabainisha faida za kupata chanjo dhidi ya COVID-19, "amesema Edouard Beigbeder, Mwakilishi wa UNICEF nchini DRC, kulingana na radio ya kimataifa nchini DRC, OKAPI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.