Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI-CHANJO-ASTRAZENECA

Rais Tshisekedi ashtumiwa kwa kutochoma chanjo ya AsraZeneca

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakati huu serikali inapoendelea na kampeni ya kuhamasisha wananchi wapate chanjo aina ya AsraZeneca, imebainika kuwa rais Felix Tshisekedi hajapata chanjo hiyo.

Rais wa DRC  Felix Tshisekedi
Rais wa DRC Felix Tshisekedi AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinsema rais huyo haamini chanjo hiyo aina ya AsraZeneca, jambo ambalo sasa linaoneka ni kinyume cha mpangp wa serikali kuwaaminisha wananchi kukubali chanjo hiyo wakati huu nchi hiyo ikikabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya Corona.

Msimamo huu wa rais Tshisekedi, umezua maswali mengi kuhusu ni vipi, yeye hataki kupata chanjo hiyo wakati serikali aliyoiongoza, ikiwataka wananchi kupata chanjo hiyo.

Aliyekuwa mgombea wa urais mwaka 2018 Martin Fayulu, ni miongoni mwa wanasiasa na watu mashuhuri  waliomkosoa rais Thisekedi kwa kile anachosema, alipaswa kuwa katika mstari wa mbele kuonesha kwa mfano kwa kupokea chanjo hiyo ya AsraZeneca.

Ukosoaji huu pia umetolewa na wanadiplomasia jijini Kinshasa.Balozi  mmoja ambaye hakutaka kutajwa amesema, Thisekedi kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, alipaswa kuonesha kwa mfano kwa kuchomwa chanjo ya AstraZeneca inayotumiwa na waafrika wengi.

Nao watalaam wa afya nchini humo wanasema hawawezi kumkosoa wazi rais Thisekedi lakini wanasikitishwa na msimamo wake, licha ya kuwahimiza wananchi kupata chanjo hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.