Pata taarifa kuu
DRC-AFYA

DRC yatangaza kukabiliwa na mlipuko wa tatu wa COVID-19

Waziri wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Jacques Mbungani ametangaza kuwa nchi hiyo kwa sasa inakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya Covid 19 huku jiji kuu Kinshasa likiathiriwa zaidi.

Raia wa DRC walioambukizwa aina mpya ya kirusi kutoka INdia wakiandamana katika sehemu waliwekwa karantini, KInshasa, Mei 19, 2021.
Raia wa DRC walioambukizwa aina mpya ya kirusi kutoka INdia wakiandamana katika sehemu waliwekwa karantini, KInshasa, Mei 19, 2021. Arsene Mpiana AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo ameeleza kuwa kwa kipindi cha wiki nne zilizopita, kumekuwa na ongezeko la maambukizi na vifo kufuatia kuwepo kwa virusi aina ya Delta kutoka India na Beta kutoka Afrika Kusini.

WHO inasema kuanzia mwezi uliopita, virusi aina ya SARS-Cov-2 vimekuwa vikishuhudiwa kwa wingi katika jiji hilo, wakati huu Waziri wa afya nchini humo Jean-Jacques Mbungani akitangaza nchi hiyo kuanza kushuhudia mlipuko wa tatu wa maambukizi hayo.

Mkuu wa WHO barani Afrika Daktari Matshidiso Moeti, anaonya kuwa DRC pamoja na mataifa mengine ya Afrika yapo katika hatari ya kuathiriwa na mlipuko wa tatu.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa upatikanaji wa chanjo barani Afrika kwa haraka ndio suluhu ya kuzuia ongezeko la maambukizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.