Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI-CHANJO-ASTRAZENECA

Ikulu ya Kinshasa yafafanua kauli ya rais Tshisekedi kuhusu chanjo ya AstraZenenca

Hatua ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi kusema hataki kupokea chanjo ya AstraZenenca, imezua hali ya sintofahamu nchini humo, wakati huu serikali yake ikiendelea na kampeni ya kuwataka wananchi kupokea chanjo hiyo ili kuzuia maambukizi ya Covid 19.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Thisekedi
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Thisekedi © AFP
Matangazo ya kibiashara

Hii imesababisha raia wengi wa taifa hilo kutojitokeza kwa wingi kupokea chanjo hiyo kwa kile kinachooneka  kuwa, hawaiamini chanjo hiyo.

Hata hivyo, Ikulu ya rais Tshisekedi, kupitia Mkurugenzi wa mawasiliano Erik Nyindu  ameiambia RFI kuwa msimamo wa  kiongizi huyo haujaeleweka na raia wengi.

Rais yupo kwenye mstari wa mbele kuhamasisha umma kupokea chanjo, kwa sababu ni chanjo inayotumiwa na mataifa mbalimbali barani Afrika.

Aliyekuwa mgombea wa urais mwaka 2018 Martin Fayulu, ni miongoni mwa wanasiasa na watu mashuhuri  waliomkosoa rais Thisekedi kwa kile anachosema, alipaswa kuwa katika mstari wa mbele kuonesha kwa mfano kwa kupokea chanjo hiyo ya AsraZeneca.

Ukosoaji huu pia umetolewa na wanadiplomasia jijini Kinshasa.Balozi  mmoja ambaye hakutaka kutajwa amesema, Tshisekedi kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, alipaswa kuonesha kwa mfano kwa kuchomwa chanjo ya AstraZeneca inayotumiwa na waafrika wengi.

Watalaam wa afya nchini humo wanasema hawawezi kumkosoa wazi rais Tshisekedi lakini wanasikitishwa na msimamo wake, licha ya kuwahimiza wananchi kupata chanjo hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.