Pata taarifa kuu
DRC-UFARANSA-COVID 19

Ufaransa yatahadharisha kuhusu kasi ya maambukizi ya Covid 19 nchini DRC

Ufaransa imeijumuisha nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo miongoni mwa nchi zenye maambukizi makubwa ya virusi vya corona aina ya Delta inayosambaa kwa kasi.

Mtaa wa Gombe jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Mtaa wa Gombe jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa inasema hali hii inazua wasiwasi na hivyo inaweka vikwazo kwa abiria wanaotokea nchini DRC kwenda nchini humo.

Hatua hii imekuja wakati huu takwimu zikionesha kuwa kufikia Juni 29, asilimia 84 ya maambukizi nchini DRC yalikuwa aina ya Delta.

Mataifa 24 duniani yakiwemo manne ya Afrika yamewekwa katika orodha hiyo na Ufaransa, hatua ambayo imechukuliwa na nchi ya Ubelgiji.

Mataifa mengine ya Afrika yaliyojipata katika orodha hiyo ya Ufaransa ni pamoja ni Afrika Kusini ambayo inasumbuliwa na virusi aina ya Beta.

Virusi vya Delta ambavyo chimbuko lake ni nchini India, pia vinaripotiwa kusambaa nchini Afrika Kusini.

Mwezi Juni, Namibia na Ushelisheli pia yaliwekwa katika kundi hilo na Ufaransa na sasa abiria kutoka nchini humo wataruhusiwa kuingia nchini humo wakiwa na sababu muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.