Pata taarifa kuu

WHO : Dunia haiko pamoja katika vita dhidi ya Corona

Shirika la Afya duniani WHO linasema linashtushwa na mataifa kushindwa kupata chanjo za kutosha kukabiliana na janga la Covid1-9, hatua ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Tedros Ghebreyesus, amewaambia Mawaziri wa afya kwenye kikao kupitia mtandao kuwa, hii inaonesha dunia haipo pamoja katika vita dhidi ya virusi hivyo.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus, anasema dunia haipo pamoja katika vita dhidi ya virusi Corona na ndio maana ugonjwa huo unaendelea.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Ghebreyesus, anasema dunia haipo pamoja katika vita dhidi ya virusi Corona na ndio maana ugonjwa huo unaendelea. Christopher Black World Health Organization/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni shirika la Afya Duniani, WHO lilizikosoa nchi tajiri duniani kwa kuanza kutoa chanjo ya tatu ya nyongeza ya COVID-19, huku mamilioni ya watu katika nchi masikini wakiwa bado hawajapata hata dozi moja ya chanjo. 

Wataalamu wa WHO wanasema hakuna ushahidi wa kutosha wa kisayansi unaoonesha kwamba chanjo za nyongeza zinahitajika kwa watu ambao tayari wamechanjwa mara mbili, na iwapo hilo litafanikisha kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.

Hata hivyo Mkurugenzi wa masuala ya Dharura wa WHO, Mike Ryan alisema ukweli wa kimsingi na kimaadili ni kwamba wanataka kuwaokoa kwa mara ya pili watu, huku wakiwaacha mamilioni ya watu bila msaada wowote wa kuwalinda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.