Pata taarifa kuu

WHO: Dozi ya 3 ya chanjo dhidi ya Corona sio lazima kwa sasa

Kusambaa kwa aina mpya ya kirusi Corona, Delta, katika maeneo yenye viwango vya chini vya chanjo inakuza maambukizi ya COVID-19 ulimwenguni kote, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Jumatano hii, na kuagiza kukamilisha chanjo kamili katika maeneo hayo, kabla ya kuzindua kampeni za kukumbusha katika nchi zenye mapato ya juu.

Kulingana na WHO, kipaumbele kinapaswa kutolewa kwa chanjo kamili katika maeneo yenye viwango vya chini vya chanjo, kwa sababu ya ukosefu wa takwimu zinayothibitisha kwamba dozi ya tatu ya chanjo ni muhimu.
Kulingana na WHO, kipaumbele kinapaswa kutolewa kwa chanjo kamili katika maeneo yenye viwango vya chini vya chanjo, kwa sababu ya ukosefu wa takwimu zinayothibitisha kwamba dozi ya tatu ya chanjo ni muhimu. AP - Martial Trezzina
Matangazo ya kibiashara

"Kirusi cha Delta yenyewe, kinazunguka katika maeneo ambayo kiwango cha chanjo kiko chini na katika mazingira ya matumizi madogo na yasiyolingana na afya ya umma na hatua za kijamii," amesema mtaalam wa magonjwa kutoka Shirika la Afya Duniani, Maria Van Kerkhove, katika mkutano wa waandishi wa habari huko Geneva.

Chanjo hizo huzuia wazi kuongezeka kwa aina kali za ugonjwa na vifo vinavyosababishwa na kirusi cha Delta, ameongeza mwanasayansi mkuu wa WHO Soumya Swaminathan.

Kulingana na WHO, kipaumbele kinapaswa kutolewa kwa chanjo kamili katika maeneo yenye viwango vya chini vya chanjo, kwa sababu ya ukosefu wa takwimu zinayothibitisha kwamba dozi ya tatu ya chanjo ni muhimu.

Taarifa hizi zinakuja kabla tu ya serikali ya Marekani kutangaza nia yake ya kutoa chanjo kwa kuchomwa sindano za nyongeza kwa Wamarekani wote kuanzia Septemba 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.