Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-AFYA

Ramaphosa kushirikiana na nchi za afrika ili kutengeneza chanjo ya Covid 19

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema nchi yake kwa kushirikiana na mataifa mengine barani Afrika, yameanza hatua ya kutenegeza chanjo za kuzuia maambukizi ya Covid 19  kwa ajili ya taifa lake na bara la Afrika.

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa akipokea chanjo yake ya kwanza aina ya Johnson and Johnson katika Hospitali ya Khayelitsha karibu na Cap, February 17 2021.
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa akipokea chanjo yake ya kwanza aina ya Johnson and Johnson katika Hospitali ya Khayelitsha karibu na Cap, February 17 2021. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Mradi huu unaungwa mkono na kampuni mbalimbali za dawa nchini Afrika Kusini na kuungwa mkono na Umoja wa Afrika na Shirika la Afya duniani.

Aidha, Ramaphosa amesema ni aibu kwa mataifa tajiri kuendelea kuhifadhi chanjo wasizozitumia wakati mataifa ya Afrika yakihangaika.

Ramaphosa ameongeza kuwa chanjo ambazo zimetengenezwa kwa kutumia mabilioni ya pesa na mataifa tajiri wakati mataifa mengi ya Afrika hayana uwezo wa kuzipata licha ya kwamba mataifa hayo yana akiba kubwa.

Kurasimisha chanjo lazima hatua hii ifike mwisho kwa kuwa tunakabiliwa na janga hili wote duniani, sio sawa kabisa kwamba baadhi ya watu duniani kwa sababu wanatokea kwenye mataifa tajiri basi maisha yao ni muhimu na ya thamani kuliko wale wanaotokea kwenye mataifa masikini.amesisitiza rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.