Pata taarifa kuu
WHO-AFYA

Covid-19: WHO yaomba maabara kugawana 50% ya chanjo zao na Covax

Shirika la Afya Duniani, WHO, imeomba watengenezaji wa chanjo dhidi ya CoOVID-19 kuweka nusu ya uzalishaji wao kwa utaratibu wa kimataifa wa kugawana na mpango wa Covax mwaka huu. Huu i wito mwingine wa mshikamano - baada ya shirika hilo kukata tamaa kidogo , na saxa inategemea kwa kiasi kikubwa ishara mpya kutoka kwa nchi zilizostawi zaidi kiviwanda duniani G7 mwishoni mwa wiki hii.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anakumbushaa kwamba nchi masikini zimepokea tu 0.4% ya chanjo zinazotolewa duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anakumbushaa kwamba nchi masikini zimepokea tu 0.4% ya chanjo zinazotolewa duniani. Christopher Black World Health Organization/AFP
Matangazo ya kibiashara

Je! Inawezekana kushawishi maabara ya Pfizer-BionNTech, Moderna au AstraZeneca kuhifadhi chanjo zao kwa nchi ambazo zinazihitaji zaidi? Kisheria, inaonaeka kuwa ngumu. Lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) bado iliomba siku ya Jumatatu, watengenezaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 kukataa maagizo mapya, au kwa hali yoyote kutoa 50% ya dozi zao kwa Covax, mpango wenye dhamana ya usambazaji sawa wa chanjo kwa nchi masikini.

Kuanzia Juni 4, dozi milioni themanini zilikuwa zimesambazwa bila malipo na Covax katika nchi 129. Hii ni mara mbili hadi tatu chini ya ile iliyotarajiwa na WHO kufikia sasa. Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Ghebreyesus anatukumbusha mara kwa mara kwamba nchi masikini zimepokea tu 0.4% ya chanjo zinazopewa duniani, dhidi ya karibu nusu kwa nchi tajiri. “Kinachokatisha tamaa zaidi kuhusu takwimu hizi ni kwa sababu hazijabadilika kwa miezi kadhaa. Ukosefu wa usawa wa chanjo ni tishio kwa nchi zote. Sio wale tu ambao hawana chanjo, ”Tedros Ghebreyesus alisema Jumatatu wiki hii.

Wito kwa G7

Mwezi Mei, Mkutano Mkuu wa Afya duniani, Dk Tedros alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchanja angalau 10% ya raia kwa kila nchi ifikapo mwezi Septemba na angalau 30% ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. "Ili kufikia malengo haya, tunahitaji dozi milioni 250 za ziada ifikapo mwezi Septemba, na dozi milioni 100 mwezi Juni na Julai pekee," alikumbushaa mkuu wa WHO. Wikiendi hii, viongozi wa nchi za G7 watakutana kwa mkutano wao wa kila mwaka. Mataifa haya saba yana uwezo wa kufikia malengo haya. Ninaomba G7 ijitolee sio tu kugawana dozi, bali pia kuawana chanjo katika mwezi wa Juni na Julai, ”alisema.

WHO inatumai nchi tajiri zitafuata mfano huo na Marekani. Joe Biden ameahidi tu msaada wa dozi milioni 80. Robo tatu itapewa Covax. Huu ni msaada mkubwa zaidi wa aina yake tangu kuzuka kwa janga hilo.

Marekani, pia sasa inapendelea kufutwa kwa hati miliki kwenye chanjo na matibabu kama inavyodaiwa na nchi sitini, ikiwa ni pamoja na India na Afrika Kusini. Mada hii inatarajia kujadiliwa tena mbele ya WTO mumanne 8 Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.