Pata taarifa kuu
AFRIKA-AFYA

WHO: Idadi ya vifo yaongezeka kwa 43 % kwa wiki moja barani Afrika

Idadi ya vifo vinavyosababishwa na COVID-19 imeongezeka kwa asilimia 43 barani Afrika wiki iliyopita, ambapo nchi nyingi zinakabiliwa na uhaba wa oksijeni ya matibabu na vitanda kwa wagonjwa mahututi kukabiliana na kuongezeka kwa maambukizi, huku kukiripotiwa uhaba wa chanjo, Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema.

Makao makuu ya shirika la Afya Duniani, WHO, Geneva, Mei 19, 2020.
Makao makuu ya shirika la Afya Duniani, WHO, Geneva, Mei 19, 2020. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Kwa wiki tano idadi ya vifo ikiwa juu, ripoti ya idadi ya vifo kutokana na COVID-19, vilivyorekodiwa rasmi, ilifikia 6,273 wiki iliyopita barani Afrika, idadi inayokaribia ile ya wezi Januari mwaka huu, na idadi ya maambukizi sasa ni zaidi ya milioni sita.

Kiwango cha vifo nchini Afrika kinafikia kwa 2.6% ikilinganishwa na wastani wa asilimia 2.2%, ofisi ya WHO barani Afrika imesema katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari

Kulingana na WHO, vifo vingi vimerekodiwa Namibia, Afrika Kusini, Tunisia, Uganda na Zambia.

Kuongezeka kwa maambukizi, ambayo kwa sehemu imetokana na uwepo wa aina mpya ya kirusi cha Delta, kinachambukiza haraka, katika nchi 21 za afrika, imesababisha "vifo vingi," amesema Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa WHO barani Afrika.

"Hii ni bendera nyekundu kuwa hospitali katika nchi zilizoathirika zaidi zinafikia hatua," aliongeza.

Ilichukua mwezi mmoja tu kwa maambukizi kuongezeka kwa milioni moja, wakati ingelichukua miezi mitatu kuongezeka kutoka milioni 4 hadi milioni 5, amesema Matshidiso Moeti.

Afrika inakabiliwa na shida za usambazaji wa chanjo na ni dozi milioni 53 tu ambazo zimetolewa hadi sasa, ameongeza. Kati ya jumla ya watu bilioni 1.3, watu milioni 18 tu ndio wamepewa chanjo kamili barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.