Pata taarifa kuu
MAREKANI-UINGEREZA-OBAMA

Uingereza: ziarani London, Obama aomba kutojiondoa katika EU

Rais Barack Obama amesema anaunga mkono Uingereza kubaki na kuondelea na mchango wake katika Umoja wa Ulaya hasa katika vita dhidi ya ugaidi na masuala ya wahamiaji na utatuzi wa migogoro ya kiuchumi.

Rais wa Marekani Barack Obama akiwasili katika uwanja wa ndege wa Stansted, London, Aprili 21, 2016.
Rais wa Marekani Barack Obama akiwasili katika uwanja wa ndege wa Stansted, London, Aprili 21, 2016. REUTERS/Peter Nicholls
Matangazo ya kibiashara

Rais Obama amenukuliwa na gazeti la Uingereza Telegraph, akisema kwamba uanachama wa Uingereza katika umoja wa Ulaya una umuhimu mkubwa na endapo nchi hiyo itajiondoa katika umoja huo itapunguza nguvu katika vita dhidi ya ugaidi duniani, suala la wahamiaji na utatuzi wa matatizo ya kiuchumi.

"Nasema kwa moyo mkunjufu kwa mtu kama rafiki, kwamba matokeo ya uamuzi wako ni wa maslahi ya kina kwa Marekani," ameandika rais wa Marekani. "Umoja wa Ulaya haupunguza ushawishi wa Uingereza, bali unaongeza," Obama amehakikisha. "Kwa hiyo Marekani na dunia wana haja ya ushawishi wako mkubwa kuendelea, ikiwa ni pamoja na katika Umoja wa Ulaya," Obama amesema, na hivyo kujikubalisha kusaidia katika kampeni inayoendelea ya kura ya maoni.

Zaidi ya Wabunge mia moja kutoka chaa cha conservative ambao wanataka Uingereza ijiondoe katika Umoja wa Ulaya pia wamemuandika Balozi wa Marekani mjini London wakipinga mwenendo wa Rais Obama wa"kuingilia kati" masuala ya Uingereza.

Rais wa Marekani leo Ijumaa anatazamiwa kuchangia chakula cha mchana na malkia Elizabeth II na kukutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon. Mazungumzo yao yatajikita hasa katika suala zima la ushirikiano kati ya mataifa hayo na pamoja na Umoja wa Ulaya na vita dhidi ya ugaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.