Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA WA NYUKLIA

Mkutano wa Washington kuzungumzia tishio la kijihadi

Katika mkutano wa kilele juu ya usalama wa nyuklia, Rais Obama alikuwa na mikutano kadhaa na wakuu mbalimbali wa nchi na serikali. Korea ya Kaskazini iliku moja ajenda mazungumzo yake na Rais wa Korea Kusini na Waziri Mkuu wa Japan.

Rais wa Marekani Barack Obama (kushoto) alizungumza na mwenzake wa Ufaransa Francois Hollande, Machi 31, 2015, Washington.
Rais wa Marekani Barack Obama (kushoto) alizungumza na mwenzake wa Ufaransa Francois Hollande, Machi 31, 2015, Washington. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Mada hii pia ameijadili na Rais wa China. Katika mkutano na Rais François Hollande, walizungumzia hasa mapambano dhidi ya ugaidi wa wanamgambo wa Kiislamu.

Marais na viongozi wa serikali pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wanaoshiriki mkutano kuhusu usalama wa nyuklia mjini Washington watajadili Ijumaa hii, kuhusu hasa tishio la kundi la Islamic State (IS) katika nyanja hii. Jana, Alhamisi, Machi 31, walizungumzia kuhusu uchokozi wa Korea ya Kaskazini.

Mbali na mazungumzo ya leo, kuna mkutano uliofanyika kati ya marais wa Ufaransa na Marekani. Barack Obama amekaribisha kazi inayofanywa na François Hollande katika mapambano dhidi ya kundi la Islamic State: "Rais Hollande alikua kiongozi katika kuhamasisha jumuiya ya Ulaya juu ya haja ya kuwa na ufanisi zaidi katika kubadilishana taarifa katika ukanda huo."

Rais wa Ufaransa, kwa upande wake, amekaribisha uratibu wa "kiwango cha juu" kati ya Ufaransa na Marekani katika suala la ujasusi na ufuatiliaji wa wapiganaji wa kigeni.

Muungano wa kimataifa dhidi ya kundi la IS unapaswa kuiruhusu serikali ya Iraq kurejesha kwenye himaya yake maeneo yote, ikiwa ni pamoja na Mosul. Nchini Syria, aliendelea, Ufaransa inachangia kwa suala la msaada wa kijeshi, lakini pia kisiasa, "Tunaamini kwamba Daech imeanza kupoteza katika uwanja wa vita, na kwa mtazamo huu, Raqqa [ngome ya IS nchini Syria] ni lengo letu."

Obama akutana na Erdogan

Aidha, kundi la Islamic State pia liligubikwa katika mazungumzo kati ya Rais wa Marekani, na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. "Rais wa Marekani ametoa rambirambi zake kwa Rais Erdogan kwa niaba ya watu wa Marekani kwa watu waliouawa na kujeruhiwa katika shambulio la kigaidi mjini Diyarbakir na amethibitisha uungwaji mkono wa Marekani kwa nchi ya Uturuki," Ikulu ya White House imeema. Siku ya Alhamisi, shambulio la bomu liliotegwa ndani ya gari, liliwaua watu saba, wote askari polisi, na kujeruhiwa watu 27 katika mji wa Diyarbakir, kusini mashariki mwa Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.