Pata taarifa kuu
MALI-EBOLA-Afya

Mali : mtu wa kwanza abainika kuwa na virusi vya Ebola

Mali imeorodhesha mtu wa kwanza kubainika kuwa na virusi vya Ebola , ambaye ni msichana mdogo aliye ingia Mali akitokea nchi jirani ya Guinea. Msichana huyo amewekwa karantini katika mji wa Kayes, magaharibi mwa Mali, wizara ya afya imeeleza.

Wafanayakazi katika sekta ya afya wanamfanyia vipimo mtoto kwenye mpaka kati ya Guinea na Mali, Oktoba 2 mwaka 2014.
Wafanayakazi katika sekta ya afya wanamfanyia vipimo mtoto kwenye mpaka kati ya Guinea na Mali, Oktoba 2 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Msichana huyo, mwenye umri wa miaka miwili, anatokea katika mji wa Kayes magharibi mwa Mali. Aliingia Mali akitokea Guinea. Vipimo vya mwanzo vilionesha kuwa msichana huyo aliambukizwa virusi vya Ebola. Msichana huyo alikua na homa na amekua akitokwa damu puani.

Baada ya kuona dalili hizo, familia ya mtoto huyo iliharakia kumuona muuguzi ambaye mara moja aliitaka familia hiyo kuharakia hospitali haraka iwezekanavyo. Wakati huo huo viongozi wa hospitali walitoa tahadhari na kubaini kwamba mtoto huyo huenda ameambukizwa virusi vya Ebola.

Baada ya kitengo cha Idara ya huduma za dharura kupata taarifa hiyo, timu ya wataalamu ilijielekeza katika mji wa Kayes, kwenye umbali wa kilomita 600 na mji mkuu wa Mali, Bamako. Mtoto huyo alifanyiwa vipimo vya damu na kubainika kuwa aliambukizwa virusi vya Ebola.

Wizara ya afya imefahamisha kwamba mtoto huyo anaendelea vizuri baada ya kupata huduma za kutosha. Viongozi wa Mali wamesema kwamba watu waliyogusana au kuwa karibu na mtoto wamewekwa karantini na tayari wameanza kufanyiwa vipimo ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

Wizara ya afya ya Mali imewataka raia kuwa na utulivu, na kubaini kwamba viongozi wanafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha kuwa ugonjwa huo umedhibitiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.