Pata taarifa kuu
EBOLA-ULAYA-AFRIKA-AFYA

Ebola: Mawaziri 28 wa mambo ya nje wa Ulaya wakutana

Baada ya mkutano wa Mawaziri wa Afya wiki iliyopita, hatimaye Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ulaya wanakutana leo Jumatatu oktoba 20 katika mji wa Luxembourg ili kujadili kuhusu jawabu la Umoja wa Ulaya juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Abiria wakifanyiwa vipimo wanapowasili kwenye viwanjwa vya ndege vya Uingereza.
Abiria wakifanyiwa vipimo wanapowasili kwenye viwanjwa vya ndege vya Uingereza. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Liberia, nchi ambayo inaendelea kuathirika zaidi na ugonjwa huo, amesema jana Jumapili kwamba kila nchi inapaswa kufanya jitihada ili kuhakikisha kwamba imewalinda raia wake dhidi ya Ebola.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, ugonjwa wa Ebola umewaua watu zaidi ya 4500.

Mawaziri hao wa Mambo ya Nje wa Ulaya wameapa kutokomeza ugonjwa wa Ebola, hasa kusaidia mataifa yanaoendelea kuathirika kuudhibiti ugonjwa huo.

Katika mkutano huo mawaziri hao watazungumzia kuhusu jinsi ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Ebola ili usiendelei kuenea duniani.

Uingereza ambayo ni nchi ya kwanza kuchukua uamzi wa kukagua na kuchunguza katika viwanja vyake vya ndege kiwango cha joto kwa abiria wanaoingia nchini humo wakitokea Guinea, Sierra Leone na Liberia, imesema itaendelea na zoezi hilo ili kulinda raia wake dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ebola.

Viongozi hao watajaribu kutahtmini kwa pamoja utaratibu wa kuwaondoa barani Afrika raia kutoka Ulaya ambao wamebainika kuwa na virusi vya Ebola. Kwa mujibu wa wataalam, watu wawili kutoka Ulaya ambao wamebainika kuwa na virusi vya Ebola watasafirishwa Ulaya kwa wakati mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.