Pata taarifa kuu
KENYA-ICC-Haki za binadamu-Sheria

Kenya: Uhuru Kenyatta mbele ya majaji wa ICC

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewasili Hague Jumatano wiki hii, ambapo anahudhuria mbele ya majaji wa Mahakama ya Kimataifa ICC kesi inayomkabili .

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uhuru Kenyatta anatuhumiwa makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu, baada ya kushukiwa kuhusika katika machafuko yaliyotokea nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa rais tangu mwaka 2007 hadi mwaka 2008.

Jana Jumanne Mahakama ya Kimataifa ICC imekutana ili kujadili kesi hiyo. Wakati huo huo Ofisi ya Mwendesha mashtaka kwenye Mahakama ya Kimataifa imeiomba Mahakama hiyo kutambua kwamba Kenya haitowi ushirikiano wowote katika uchunguzi utakaopelekea ufunguzi wa kesi hiyo.

“ Tuko katika hali ngumu, kwani serikali ya Kenya imekataa kutoa ushirikiano wake”, mwakilishi wa mwendesha Mashtaka amesema wakati kesi hiyo ikisikilizwa.

Lengo la kauli hiyo ya mwakilishi wa Mwendesha mashtaka ni kutaka kuifahamisha rasmi Mahakama kwamba Kenya haizingatii majukumu yake ya kisheria, na hivyo kuhalalisha ombi la kuahirishwa kesi hiyo kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

Upande wa mashtaka umebaini kwamba uliomba tangu miezi kadhaa iliyopita kumbukumbu za benki na sim ili kuthibitisha jukumu la Kenyatta katika ghasia ziliyotokea mwishoni mwa mwaka 2007.

Upande wa utetezi umebaini kwamba Ofisi ya Mwendesha mashtaka haina vithibitisho vinavyoonesha kwa namna gani Kenyatta alishiriki katika machafuko hayo. Wanasheria wa Kenyatta wameomba kesi hiyo ifutwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.