Pata taarifa kuu
KENYA-ICC-Siasa-Haki za binadamu-Sheria

Kenya: rais Kenyatta awasili Hague

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewasili mjini Hague nchini Uholanzi, kuhudhuria kikao kuhusu kesi inayomkabili ya kukochechea na kufadhili machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kikao hicho kitafanyika Jumatano wiki hii, na kinakuja baada ya upande wa mashtaka kuomba majaji wa Mahakama hiyo kuahirisha kesi dhidi ya Kenyatta kwa muda usiojulikana kwa kile wanachosema serikali ya Kenya imekataa kushirikiana na Ofisi hiyo, ili kupata nyaraka muhimu zinazomuhusu rais Kenyatta kama rekodi zake za mawasiliano ya simu na taarifa zake za kifedha.

Mbali na hilo, Ofisi ya kiongozi wa Mashtaka Jumanne wiki hii imewaomba majaji wa Mahakama hiyo kuamua kuwa Kenya haishirikiani na Ofisi hiyo kuhusu kesi inayomkabili rais Kenyatta.

Rais Kenyatta, siku ya Jumatatu alikabidhi Madaraka ya urais kwa naibu wake William Ruto, ili kukaimu wadhifa huo kwa kipindi chote atakachokuwa mjini Hague.

Kenyatta aliwaambia wabunge jijini Nairobi amekwenda kuhudhuria kikao hicho kama raia wa kawaida wala sio kama rais wa Kenya.

Kiongozi huyo wa Kenya ameendelea kusisitiza kuwa hakufadhili wala kuchochea machafuko hayo yaliyosababisha zaidi ya watu elfu moja kupoteza maisha na maelfu kuyakimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.