Pata taarifa kuu
KENYA-ICC-UPINZANI-Siasa-Haki za binadamu

Kenya: rais Kenyatta atazamia kulihutubia Bunge

Rais Uhuru  Kenyatta wa Kenya hivi leo  Jumatatu saa tisa mchana (saa za Afrika mashariki) anatarajwiwa kuhutubia kikao maalum cha bunge. 

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta. Reuters/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa haijulikani rais Kenyatta anatarajiwa kuwambia nini wabunge na maseneta kwenye kikao hicho ambacho  wanasiasa wa Upinzani wametangaza kukisusia.

Zaidi ya  wananchi wa Kenya milioni arobaini wansubiri kwa hamu kusikia hotuba ambayo rais Uhuru Kenyatta anatarajia kutoa kwenye kikao maalum cha wabunge na maseneta mjini Nairobi.

Hotuba hiyo ya Kenyatta inakuja siku mbili kabla ya kuelekea mjini Hague, Uholanzi ambako ameitwa na majaji watatu wanaotengewa kusikiliza kesi yake ya makosa ya jinai yanayohusiana na fujo zilizotokea mwaka 2007 baada baada ya uchaguzi wa rais.

Hadi leo jumatatu asubuhi haijulikani kama Rais Kenyatta ataelekea Hague kama alivyohitajika kuelekea katik mji huo ama atakaidi na kusalia nchini Kenya.
Ni baada ya yeye kuhutubia bunge ndipo itabainika wazi kuwa ataenda au la.

Hata hivo Makamu wa rais, William Ruto ametoa wito kwa wananchi wa Kenya kumuombea rais Kenyatta ikisubiriwa kujua kama ataenda Hague au la.

 Hata hivyo wito wa rais Kenyatta kuwataka wabunge, ambao kwa wakati huu wako likizoni kufika bungeni kwa kikao hicho maalum, umepokelewa kwa shingo upande na wabunge na maseneta wa chama cha Upinzani cha CORD, kinachoongozwa na Raila Odinga.

Ingawaje wabunge walio wachache bungeni hawajatamka lolote kuhusu kikao hicho, maseneta  kupitia kwa kiongozi wa wachache kwenye Baraza la Seneti, Moses Wetangula, wameeleza kuwa watasusia kikao hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.