Pata taarifa kuu
KENYA - SHERIA

Serikali ya Kenya yakanusha taarifa za kuendeshwa kwa matakwa ya sheria za kimataifa wala hati za mahakama ya ICC

Serikali ya Kenya kupitia mwanasheria wake mkuu imesema kuwa kamwe haiendeshwi kwa matakwa ya sheria za kimataifa wala hati za mahakama ya ICC na badala yake inafuata sheria zake za ndani kutekeleza maombi yoyote. Profesa Githu Mwigae ameyasema hayo wakati akijibu hoja za majaji wa ICC hivi mjini The Hague nchini Uholanzi.

Githu Mwigae muendesha mashtaka mkuu wa Kenya
Githu Mwigae muendesha mashtaka mkuu wa Kenya
Matangazo ya kibiashara

Akijiamini na kuzungumza kwa Staha, mwanasheria mkuu wa Serikali ya Kenya, Profesa Githu Mwigae amewaambia majaji wa mahakama ya ICC kuwa nchi yake haijakataa kamwe kushirikiana na ofisi ya mwendesha mashtaka kama inavyodai na badala yake ofisi hiyo imeshindwa kuelewa sheria za Kenya.

Alipoulizwa na majaji kwanini ofisi yake imeshindwa kuheshimu hati halali iliyotolewa na mahakama hiyo kuitaka ofisi yake kutoa ushahidi wa muhimu kwa ofisi ya mwendesha mashtaka. 

Majaji wa mahakama ya ICC pia walitaka kufahamu ni muda gani ambao serikali ya kenya itachukua kutekeleza na kisha kukabidhi nyaraka zinazotakiwa na mahakama hiyo, Profesa Mwigai aliendelea kutia ngumu na kudai kuwa hafahamu itachukua muda gani kutekeleza hilo.

Mwanasheria mkuu wa Serikali ya Kenya alilazimika kwenda kwenye mahakama hiyo kufuatia kuombwa kufanya hivyo na majaji wa mahakama ya ICC ili kufafanua ni kwanini Serikali ya Kenya imeshindwa mpaka sasa kuheshimu sheria za kimataifa zinazoitaka nchi hiyo kushirikiana na mahakama ya ICC.

Hatua hii inafuati tuhuma zilizotolewa na mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo, Fatou Bensouda kudai kuwa kukwama kwa kesi dhidi ya rais Uhuru Kenyata kunatokana na nchi hiyo kukataa kumpatia baadhi ya nyaraka muhimu ikiwemo taarifa ya fedha za rais Kenyatta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.